loader
Dstv Habarileo  Mobile
Evra: Klabu zitoe elimu kuhusu ubaguzi

Evra: Klabu zitoe elimu kuhusu ubaguzi

KLABU za soka zinatakiwa kutoa elimu kwa mashabiki wake kuhusu ubaguzi.

Hayo yamesemwa na beki wa zamani wa Ufaransa na Manchester United Patrice Evra baada ya wachezaji weusi wa England kufanyiwa vitendo vya kibaguzi baada ya kufungwa kwenye fainali za Euro 2020.

Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka walikumbana na sakata la ubaguzi baada ya kukosa mikwaju ya penalti na kufanya England ipoteze fainali hizo kwa penalti 3-2 dhidi ya Italia baada ya kumaliza mechi hadi muda wa nyongeza kwa sare ya bao 1-1.

"Kama hatutafanya kitu, ubaguzi utakuwepo siku zote kwasababu umekuwepo kwa iaka mingi, unajua tunahitaji kubadilika na ndio maana eleimu ni muhimu sana,” Evra aliiambia Sky Sports.

"Nataka klabu zote ziwekeze kwenye elimu, kukutana na mashabiki, wachezaji wazungumze na mashabiki, au kundi la mashabiki na kuwaambia wanachojihisi wanapobaguliwa kwa rangi zao.”

"Usiniambie kwamba klabu za soka haziwezi kufanya hilo, au Fifa au Uefa, kuwe na vikao vingi na mashabiki kwa hiyo wataelewa hawatakiwi kutoa sauti za nyani wakati wachezaji weusi wanapogusa mpira, wawaeleze jinsi inavyowaathiri, hilo muhimu sana.”

Kauli za kibaguzi kwa wachezaji hao kwenye mitandao ziliongozwa na mashabiki wa Uingereza wakitumia kurusa zao za mitandao mbalimbali ya kijamii.

Msemaji wa Twitter wiki iliyopita alisema walilazimika kuondoa maandiko zaidi ya 1,000 ya kibaguzi na kuzifungia akaunti zilizohusika katika jambo hilo, huku Facebook wakisema walifanya haraka kuondoa maandiko hayo kila yalipowekwa kwenye kurasa za mashabiki.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/513447274da1deb0f1e444f597e068a0.jpeg

Mambo yamaenza kuvurugika kunako klabu ya PSG, baada ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi