loader
Dstv Habarileo  Mobile
Biden: Niligundua ni Rais wa Marekani nilipokutana na Putin

Biden: Niligundua ni Rais wa Marekani nilipokutana na Putin

RAIS wa Marekani, Joe Biden amesema aligundua kuwa yeye ni Rais wa Marekani rasmi alipokutana na mshirika wake, Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Biden aliyasema hayo katika mkutano wake uliofanyika Cincinnati, Ohio nchini humo.

Alielezea kuwa, katika mkutano huo alikaa na kuangaliana ana kwa ana na Putin ndipo, alipobaini kuwa yeye sasa ni Rais wa Marekani.

“Nilijua kuwa mimi niko sawa na Putin, na anajua mimi ni nani na mimi najua yeye ni nani,” alisema Biden.

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yalifanyika Juni 16, mwaka huu, Geneva ikiwa ndio mara yao ya kwanza wakiwa wakuu wa nchi zao kukutana ana kwa ana.

Pia mkutano huo ni wa kwanza baina ya Marekani na Urusi tangu mwaka 2018.

Katika taarifa yao ya pamoja, viongozi hao walisisitiza wanakusudia kuzindua mazungumzo ya kimkakati ambayo yatakuwa makubwa na madhubuti.

Pia, kwa nyongeza nchi hizo za Marekani na Urusi zinatarajia kuanza mashauriano kwa ajili ya kugusa eneo la usalama wa mtandao, kubadilishana wafungwa na kudhibiti silaha.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/093a78bd69bbcf71e51fe17450d63681.jpeg

Waziri wa Uingereza, Boris Johnson ametengua uteuzi wa ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi