loader
Chanjo milioni 1 za kwanza za Corona zimewasili Tanzania

Chanjo milioni 1 za kwanza za Corona zimewasili Tanzania

CHANJO Milioni Moja za COVID-19 aina ya Johnson & Johnson (Janssen) Ad26 zikiwa ni msaada kutoka Marekani zimewasili nchini Tanzania kwa shirika la ndege la Emirates na Kupokelewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright katika Uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

 

Tanzania inampango wa kuchanja angalau watanzania milioni 35 zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya wakazi. Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza chanjo hizo zitolewe bure na kwa hiari.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, watu 29 tayari wamefariki kwa ugonjwa huo na wengine takribani 900 wamekwisha ambukizwa.

 

 

 

 

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi