loader
Dstv Habarileo  Mobile
SMZ yalia zana haramu za uvuvi

SMZ yalia zana haramu za uvuvi

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema uchumi wa buluu unaweza kuathirika kama wavuvi wataendelea kutumia zana haramu zilizopigwa marufuku pamoja na kuharibu matumbawe ambayo ndiyo mazalia ya samaki.

Waziri wa Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Abdalla Hussein Kombo, alisema hayo katika uzinduzi wa tafiti mbalimbali zilizofanywa zikilenga kukuza uchumi wa buluu.

Alisema licha ya elimu kutolewa, wapo baadhi ya wavuvi wanaofanya kosa la kuvua samaki kwa kutumia mitego iliyopigwa marufuku ikiwemo nyavu zenye macho madogo ambazo ni hatari kwa mazingira ya bahari kwa kuwa hunasa hata samaki wadogo wasiofaa kwa matumizi.

Aidha, alitaja athari nyingine kuwa ni uharibifu wa matumbawe ambayo ndiyo mazalia ya samaki kwa kuyang’oa na hivyo kuchangia kuwepo kwa uhaba wa samaki aina ya pweza, ngisi pamoja na kamba ambao bei yake ni nzuri.

“Zanzibar iliyokuwa nchi pekee katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambayo matumbawe yake yapo salama hivi sasa wapo wavuvi wanaotumia uvuvi wa kuzamia wamekuwa wakisababisha athari kubwa kiasi ya kuwepo kwa tishio kwa baadhi ya samaki ikiwemo kamba, ngisi na pweza,” alisema.

Kombo alisema wizara ipo katika mchakato wa kuipitia tena Sheria ya Uvuvi ya Mwaka 2010 kuona kama inakidhi mahitaji ya mabadiliko ya sekta ya uvuvi na mikakati ya kuingia uchumi wa buluu.

“Tunataka kuipitia upya Sheria ya Uvuvi kuona kama kweli inakidhi mahitaji yanayokwenda na wakati wa mabadiliko ya sekta ya uvuvi itakayowanufaisha walengwa,” alisema.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Ramadhan Mwita, alisema mikakati ya SMZ inayotokana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025 ni kutekeleza kwa vitendo uchumi wa buluu na kujikita moja kwa moja katika sekta ya uvuvi.

Alisema licha ya kwamba Zanzibar ina idadi kubwa ya wavuvi kutokana na visiwa kuzungukwa na bahari kila kona, lakini mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa ni asilimia 5.2.

“Bado hatujayafikia malengo ya kuingia katika uchumi wa buluu kwa mafanikio makubwa kwa sababu walengwa katika sekta hiyo yaani wavuvi wapo nyuma katika kipato chao kutokana na kuendesha uvuvi wa kizamani usiokuwa na tija,” alisema.

Kamishna wa Tume ya Mipango anayeshughulia sera, Dk Afuwa Mohamed, alisema wataendelea kufanya utafiti unaolenga maslahi ya wananchi

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3da6844010d4f95fc5b0399ff73c387d.jpg

SHIRIKISHO la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi