loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kampuni za simu zatoa neno mapitio tozo za miamala

Kampuni za simu zatoa neno mapitio tozo za miamala

WATOA huduma za simu nchini wamepongeza uamuzi wa wa serikali uliotolewa hivi karibuni kuhusu utaratibu wa kupitia upya kodi za miamala ya simu wakiamini kuwa ni hatua sahihi itakayoongeza chachu katika uwekezaji ndani ya sekta hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu), Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Huduma ya Simu za Mkononi Tanzania (TAMNOA), Hisham Hendi ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom amesema zaidi ya wateja milioni moja hususani walioko vijijini walisitisha kutumia huduma hiyo kutokana na ongezeko la makato ambayo alisema yalitishia uhai wa sekta ya mawasiliano nchini.

“Katika siku chache zilizopita tangu sheria ya fedha ilipoanza kutekelezwa Julai 15, miamala ya wateja ilipungua kwa asilimia 45, jambo ambalo limeathiri mapato ya kampuni za simu na hivyo kupunguza kodi kwa serikali,” Mwenyekiti huyo alisema na kuongeza:

 “Tunaishukuru serikali kwa kuona umuhimu na binafsi tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa kusikiliza kilio cha wananchi.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alifanya kikao na mawaziri pamoja na wadau wa sekta ya mawasiliano kutatua changamoto hiyo ambapo kikao hicho kilikuja na mapendekezo ya kutatua changamoto iliyojitokeza.

Timu iliyoundwa na Waziri Mkuu hivi karibuni itakaa na kampuni za simu na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuangalia mambo yote yanayohusu kodi ili kuyatafutia ufumbuzi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Emmanuel Tutuba, timu hiyo inajumuisha wataalamu kutoka BoT, Mamlaka ya Mwasailiano Tanzania (TCRA), Wizara za Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mtendaji huyo alisema kuwa ana imani na matokeo na mapendekezo ambayo yatatolewa na timu hiyo iliyoundwa na Waziri Mkuu huku akisisitiza kuwa kampuni za simu zitakuwa na uwezo mkubwa kibiashara nchini.

Alisema Tanzania inajivunia ukuaji wa uchumi barani Afrika kutokana na uwekezaji mkubwa wa kampuni za simu.

Takwimu za masuala ya mawasiliano zilizotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Masuala ya Mawasiliano (GSMA), kunapokuwa na huduma nafuu za mawasiliano popote duniani, kuna uwezekano mkubwa wa kuboresha seka mbalimbali hasa ya kilimo na afya.

Hivi karibuni, Bunge lilipitisha sheria ambayo ilitoa tozo ya kodi ya miamala ya simu ambayo imesababisha malalamiko

kutoka kwa wadau wa mawasiliano, jambo ambalo lilimfanya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda timu ya wataalamu kushughulikia suala hilo.

Wiki iliyopita, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Mpango aliueleza umma kwamba Rais Samia amesikiliza kilio cha wananchi na kutoa maelekezo ya namna ya kushughulikia suala hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eadf9e7408e83a339d91d57109698056.jpg

SHIRIKISHO la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi