loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simba iko tayari kumuuza Miquissone

Simba iko tayari kumuuza Miquissone

KLABU ya Simba imesema iko tayari kufanya biashara na timu yoyote itakayomuhitaji mchezaji wake Luis Miquissone.

Miquissone ni miongoni mwa wachezaji waliotajwa kuwaniwa na mabingwa wa Ligi ya Afrika Al Ahly ikielezwa iko tayari kuweka mezani Sh bilioni mbili kuinasa saini yake.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu masuala mbalimbali, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Salim Abdallah ‘Try again’ alisema bado hawajapokea ofa juu ya mchezaji huyo ila ikitokea klabu yenye uwezo wako tayari kufanya biashara.

“Mwenye uwezo aje, sisi tunafanya biashara,”alisema na kuongeza kuwa wanajipanga tena kurudi katika ubora wa hali ya juu kwa kuhakikisha wanasajili wachezaji kulingana na hitaji la benchi la ufundi.

Alisema wanasubiri kupewa tathmini ya benchi la ufundi kujua sehemu zenye mapungufu na kuzifanyia kazi mapema kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Abdallah alisema malengo waliyonayo ni kuwa mabingwa wa Afrika baada ya miaka miwili ijayo. Katika hatua nyingine, Simba imejazwa Sh. milioni 100 na wadhamini wao Sportpesa baada ya kuchukua mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e06dd9ec88c1df4c588ceeb14d699bd5.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi