loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kamwaga achukua nafasi ya Manara Simba

Kamwaga achukua nafasi ya Manara Simba

KLABU ya Simba imemteua Mwanahabari mkungwe, Ezekiel Kimwaga kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo kwa kipindi cha miezi miwili baada ya Haji Manara kuondoka Simba na kuachia nafasi hiyo.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo imesema kuwa katika kipindi hicho cha miezi miwili Kamwaga atashiriki katika maboresho ya muundo wa utendaji wa Idara hiyo akiwa ni Mwandishi wa Habari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 kwenye tasnia ya habari akifanya kazi katika Vyombo vya Habari vya ndani na Kimataifa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kamwaga anaijua vizuri Klabu ya Simba na historia yake kwani amewahi kuitumikia katika nafasi za Msemaji wa Klabu na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba. 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/808f09363e285cc0e7b2c110a455c7a9.jpeg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi