loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kagere atoa ya moyoni Simba

Kagere atoa ya moyoni Simba

MSHAMBULIAJI wa Simba Meddie Kagere amesema pamoja na msimu uliopita kuwa na changamoto nyingi kwake, lakini anafurahi kuona timu yake ikitetea mataji yote matatu kama walivyokusudia mwanzoni mwa msimu.

Simba imeendeleza utemi wake iliyouanza misimu mitatu ya nyuma baada ya msimu huu kutetea mataji yote makubwa ya michuano ya ndani ambayo ni Ligi Kuu na Kombe la FA.

Akizungumza na gazeti hili Kagere alisema haikuwa kazi rahisi sana kama ambavyo watu wanadhani na hiyo ilitokana na mafanikio yao kwenye misimu iliyopita lakini walijipanga na kuhakikisha wanafanikiwa kitimiza malengo yao.

“Ingawa nimepita katika wakati mgumu tangu nijiunge na Simba, lakini nafurahi kwa mafanikio haya, ambayo yameonesha dhamira ya kila mmoja wetu katika kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika,” alisema Kagere.

Mshambuliaji huyo aliyemaliza msimu huu akifunga mabao 14 kwenye Ligi Kuu, alisema baada ya msimu kumalizika anarudi kwao Rwanda kwa mapumziko na kujipanga kwa ajili ya msimu mpya ingawa bado hajajua kama atakuwa sehemu ya timu hiyo.

Kagere alisema mkataba wake wa kuimtumikia Simba umamalizika baada ya ligi kuisha ingawa tayari alishaanzisha mazungumzo na uongozi wa timu hiyo kuhusu kusaini mkataba mpya, lakini mazungumzo hayo yalisimama wakati ligi ikielekea ukingoni akiahidiwa wataendelea baada ya mchezo wa fainali ya FA.

Kagera ndiye alikuwa mfungaji bora katika misimu miwili iliyopita kabla ya msimu huu kuchukuliwa na John Bocco pia wa Simba.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/199856526a149d86771a698380ff361e.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi