loader
Dstv Habarileo  Mobile
Gekul kufunga netiboli taifa leo

Gekul kufunga netiboli taifa leo

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mashindano ya Klabu Bingwa ya Taifa ya Netiboli yanayofi kia tamati kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha leo.

Gekul atashuhudia mchezo kati ya JKT Mgulani dhidi ya Tamisemi, ambapo mshindi ndiye atakuwa bingwa baada ya timu hizo hadi sasa zote kutofungwa katika mechi zao zilizotangulia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Judith Ilunda alisema jana kuwa Gekul amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika ufungaji huo wa mashindano hayo yaliyoanza wiki iliyopita.

Ilunda akielezea msimamo wa mashindano hayo hadi jana alisema, JKT Mbweni ina pointi 14 na tayari ilikuwa imebakisha mechi moja dhidi ya Tamisemi, ambayo ilikuwa na pointi 12 ilibakisha mechi mbili.

JKT Mbweni ilikuwa imefunga mabao 474 wakati wa pinzani wao wakubwa katika mbio za ubingwa Tamiseni walikuwa wamefunga mabao 372 huku mchezo wa leo kati ya timu hizo mbili, ndio utaamua bingwa nani kati ya timu hizo.

Ilunda alisema kuwa timu saba zimeshindwa kushiriki timu hizo na zile ambazo hazitoa sababu zitashuka daraja na kucheza Ligi Daraja la Pili Taifa.

Alizitaja timu ambazo ziko katika hatari ya kushushwa daraja baada ya kutotoa taarifa za kutoshiriki kwao ni pamoja na JKT Makotopola, Jiji Tanga, Polisi Tanga, Udom, Tarime Queens na Mabibo Queens.

Alisema timu ambazo hazitashushwa daraja licha ya kutoshiriki baada ya kutoa sababu ni pamoja na Nyika Queen ambao walilipa ada lakini hawakushiriki sababu ya kutokuwa na fedha, na Jeshi Stars walitoa taarifa wachezaji wake wengi kuwa wajawazito na kubaki na wachezaji wanne tu.

Naye Yasinta Amos anaripoti kuwa, timu ya wanaume ya Smart Boys imetwaa ubingwa wa Klabu Bingwa ya Taifa ya Netiboli baada ya kumaliza ya kwanza kwa upande wa wanaume.

Mashindano ya netiboli taifa yanafanyika jijini Arusha yakihusisha timu 12 za wanawake na nne za wanaume yalianza kutimua vumbi Julai 18 ambapo rasmi yatahitimishwa Julai 29 mwaka huu.

Smart Boy wametwaa ubingwa baada ya kujikusanyia pointi sita ikifuatiwa na Muungano kutoka Dodoma ikiwa na pointi nne wakati watatu ni Hapa Kazi ya Dar es Salaam ikiwa na pointi mbili na Arusha City ikishindwa kupata pointi hata moja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/70ecf7baec401d3187e874cde894d674.JPG

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi