loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania U23, Burundi fainali leo

Tanzania U23, Burundi fainali leo

FAINALI ya michuano ya kombe la  Chalenji ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, inatarajiwa kuchezwa leo kati ya Tanzania na Burundi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia kunakofanyika michuano hiyo.

Tanzania iliingia fainali baada ya kuitoa Sudan Kusini katika mchezo wa nusu fainali kwa bao 1-0, huku Burundi ikiitoa Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kutoka suluhu.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa kila timu kutokana na ubora wa pande zote mbili zikitoka kuongoza  makundi A na B.

Tanzania ilionesha ubora katika safu ya ulinzi, ikiwa imeruhusu bao moja pekee kwenye nyavu zake na kufunga matatu katika michezo mitatu iliyopita.

Kwa upande wa Burundi, imefunga mabao manne na kuruhusu moja hivyo kazi haitakuwa nyepesi kwani wote wanaonekana wako vizuri.

Mchezaji hatari wa kuchungwa wa Burundi ni Issa Hakizimana ambaye amefunga mabao mawili katika michuano hiyo mpaka sasa.

Atakayeibuka bingwa wa michuano hiyo ni yule aliyejiandaa kimbinu na kiufundi dhidi ya mwenzake.

Mara ya mwisho Tanzania kuchukua kombe hilo ni mwaka 2010 huku Burundi ikiwa haijawahi kuchukua zaidi ya kuishia nafasi ya pili mwaka 2013.

Timu tisa zilishiriki michuano hiyo ambazo ni  Tanzania Bara, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eritrea, DR Congo, Sudan Kusini na Djibouti zilizogawanywa kwenye makundi matatu yenye timu tatu tatu kila moja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/121c926447f99884a05e22433afad76f.jpeg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi