loader
Dstv Habarileo  Mobile
ATCL kutanua mbawa zaidi

ATCL kutanua mbawa zaidi

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kuanzia mwaka 2018-2022, imelenga kupanua safari zake za ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa njia yenye tija ya kibiashara.

Hayo yalibainishwa na Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi wakati wa kupokea ndege ya tano mpya aina ya Bombardier Dash 8-Q400 iliyowasili kutoka Canada.

Kuwasili kwa ndege hiyo ku- nafanya ndege zote mpya zilizo- nunuliwa na serikali kufikia tisa na nyingine mbili aina ya Airbus A220-300 zinatarajiwa kuwasili Oktoba mwaka huu.

Ndege hiyo ilipokewa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyeambatana na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, mawaziri na viongozi wengine wa serikali, chama na dini pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakion- gozwa na mkuu wa mkoa, Amos Makalla.

Matindi alisema uzalishaji wa madini, utalii na mazao ya kilimo, samaki na mbogamboga unafanya umuhimu wa kuwepo kwa safari za kikanda na kima- taifa katika kuyafikia masoko.

Kuhusu mafanikio ya ATCL, Matindi alisema kampuni hiyo imefanikiwa kurejeshewa uanachama katika mashirika ya usafiri wa anga ya kimataifa Afrika, kurejeshwa katika mfumo wa kimataifa wa uuzaji wa tiketi na kufanya tiketi za ATCL zipatikane duniani kote, kukidhi vigezo vya ukaguzi wa ubora wa usalama na uendeshaji wa utoaji wa huduma ya usafiri wa anga unaosimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Usafiri wa Anga (AITA).

Mafanikio mengine ni kuwa na mifumo rafiki ya uuzaji wa tiketi kupitia mawakala na ofisi za ATCL na kuwa na mfumo mzuri wa udhibiti wa mapato na matumizi ya fedha, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.

“Ushahidi wa maboresho haya ni uwezo wetu wa kumudu gharama za uendeshaji bila kutegemea ruzuku ya serikali,” alisema Matindi.

Kuhusu changamoto zinazoikabili ATCL, Matindi alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na madeni yaliyorithiwa na kampuni hiyo yanayofanya washindwe kupanua mtandao wa safari zao, muundo wa umiliki wa ndege unaohusisha serikali
na kufanya ATCL ihusishwe na madeni ya serikali pamoja na changamoto ya Covid-19 iliyo- punguza idadi ya abiria wakati gharma za uendeshaji zikiwa palepale.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho alisema mpango wa ATCL ni kuongeza vituo vya urukaji ikiwemo Lubumbashi, Dubai, Ndola, Muscat, London na Nairobi.

Ndege hiyo aina ya Bomba- dier Dash 8-Q400 ina uwezo wa kubeba abiria 76 na maalumu kwa safari za masafa mafupi za ndani. Imetengenezwa nchini Canada.

foto
Mwandishi: Na Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi