loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mbombo atua Azam

Mbombo atua Azam

KLABU ya Azam FC imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Idris Mbombo kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji huyo amewahi kuzigonganisha klabu za Simba na Yanga msimu uliopita lakini sasa Azam FC ndio wamefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Akizungumza na gazeti hili Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin, ‘Popat’ alisema walikuwa wakimfukuzia mshambuliaji huyo kwa muda mrefu na anafurahi kuona juhudi zao zimefanikiwa baada ya kumtambulisha kutoka timu ya El Gouna ya Misri.

“Haikuwa kazi kumpata Mbombo sababu amewahi kufanya kazi na kocha wetu George Lwandamina wakiwa Zesco United, imani yetu ataongeza nguvu kwenye kikosi chetu msimu ujao na kutufikisha pale ambako tunapakusudia kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Popat.

Popat alisema bado zoezi la usajili linaendelea na sasa wanageukia usajili wa ndani baada ya kusajili wachezaji watano wa kimataifa tangu usajili ulipofunguliwa Julai 19.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni ni Charles Zulu, Paul Katema na Rogers Kola wote raia wa Zambia mwingine ni Kenneth Muguna raia wa Kenya na mzawa Edward Manyama.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8fe80d89cbdc0aa40ba86b125ca6b255.jpg

MSANII wa muziki wa singeli, Sholo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi