loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waendesha Baiskeli 42 waanza safari ya Kilometa 6000, siku 55 Afrika Mashariki

Waendesha Baiskeli 42 waanza safari ya Kilometa 6000, siku 55 Afrika Mashariki

WAENDESHA baiskeli 42 wameanza mbio za kuhamasisha ushirikiano ndani ya Afrika Mashariki katika mashindano ya Nne maalufu‘Great African Cycling Safari’ na wanatarajiwa kupita katika majiji sita kabla ya kuhitimisha mashindano hayo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amezindua mashindano hayo Jijini Dar es Salaam na kusema ni muhimu kwa jumuia.

Washiriki hao watakimbiza baiskeli kwa zaidi ya kilomita 6000 kwa kupita katika Miji Mikuu ya Mataifa hayo ikiwemo, Dodoma (Tanzania), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda), Kigali (Rwanda) na Bujumbura (Burundi). Mashindano yatahitimishwa Jijini Arusha.

 “Hii ni alama kubwa ya ushirikiano kwa nchi za Afrika Mashariki na zaidi yanahimarisha ushirikiano wetu, sisi kama viongozi wa Jumuiya tunaona kwa namna gani ya kuishauri Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuyaweka mashindano haya katika kalenda yake ili pamoja na mambo mengine yawe katika utaratibu unaotambulika” amesema Mbarouk.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, amesema mashindano hayo yatasaidia kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo katika nchi za Afrika Mashariki sambamba na kuwavutia watu wengi zaidi kuja na kushiki mashindano hayo.

Amesema mashindano ‘Great African Cycling Safari’ yanayohusisha umbali wa Kilomita 6000 yakitumia siku 55, yana mvuto zaidi ya yale yanayojulikana kama ‘France De Tour’ ya nchini Ufaransa ambayo huusisha umbali wa Kilomita 3000 huku yakitumia siku 12 za mashindano.

 

 

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/08d75c0ecf899beb22a026c71776b311.jpeg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi