loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia atumbua wakurugenzi 54

Samia atumbua wakurugenzi 54

WIZARA ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa siku tano kuanzia leo kwa wakurugenzi wapya wa majiji, manispaa, miji na halmashauri za wilaya wafi ke kwenye vituo vya kazi kuanza kutekeleza majukumu yao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amewataka wakurugenzi hao waende kuripoti kwa makatibu tawala wa mikoa kwenye mikoa husika.

Rais Samia Suluhu Hassan juzi ameteua jumla ya wakurugenzi 184, na kwa mujibu wa Ummy, 70 kati ya hao wamehamishwa kutoka vituo vyao vya kazi na 45 wamebaki walipokuwa.

“Aidha, katika idadi hiyo wakurugenzi 69 ni wapya wakiwemo 15 walioteuliwa kujaza nafasi 54 zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa wakurugenzi katika nafasi hizo kutenguliwa,” alisema Ummy alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Ummy alisema miongoni mwa wakurugenzi wapya, 33 sawa na asilimia 48 ni wanawake na hivyo kufanya idadi ya jumla ya wanawake wakurugenzi kufikia 55 sawa na asilimia 29 ya wakurugenzi wote nchini.

Alisema wakurugenzi wawili ambao majina yameonekana kutokea kwenye maeneo zaidi ya moja wanapaswa kwenda kuripoti kwenye kituo ambacho jina limeonekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya uteuzi.

Alisema pale ambapo jina limejirudia patatambulika kama nafasi wazi na itajazwa baadaye na akazitaja nafasi hizo ni Halmashauri ya Mji wa Misungwi na Njombe.

Ummy aliwataka wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa waende kuripoti kwa makatibu tawala wa mikoa waliyokuwa wakivifanyia kazi ili wapangiwe majukumu mengine kwa kuwa bado ni watumishi wa umma.

Wakurugenzi wapya walioteuliwa na maeneo yao ya kazi ni Zainab Mwakwiya (Meru), Selemani Msumbi (Arusha), Karia Rajabu (Karatu), Hanifa Hamza (Manispaa ya Kinondoni) na Elihuruma Mabelya (Manispaa ya Temeke).

Yusuph Semwaiko (Kondoa), Paul Sweya (Mji Kondoa), Siwema Juma (Chemba), Mwanahamisi Ally (Mpwapwa), Mandia Kihiyo (Chato), Husna Chambo (Nyangh’wale), Zahara Michuzi (Mji wa Geita), Happiness Laizer (Mji Mafinga), Zaina Mlawa (Mufindi), Sophia Kambuli (Manispaa ya Mpanda), Teresia Irafay (Mlele), Shaba Juma (Tanganyika), Dollar Kusenge (Mji Kasulu), Rose Manumba (Kigoma) na Deocles Murushwagire (Kibondo).

Zainab Mbunda (Uvinza), Essau Ngoloka (Buhigwe), Athamani Msabila (Kigoma Ujiji), Kastori Msigala (Moshi), George Mbilinyi (Mtama), Tina Sekambo (Liwale), Chionda Mfaume (Nachingwea) na Emmanuel Mkonongo (Mji Bunda), Patricia John (Butiama), Amede Ngwadidako (Jiji la Mbeya), Saida Mahungu (Ulanga), Lena Nkaya (Mji Ifakara), Joanfaith Kataraia (Malinyi), Elias Mtiruhungwa (Mji Masasi) na Shamim Mwariko (Mji Newala).

Ibrahim Mwanauta (Nanyamba), Binuru Shekidele (Sengerema), Paulo Malaga (Buchosa) na Happiness Msanga (Kwimba), Maryam Muhaji (Wanging’ombe), Sharifa Nabarang’anya (Njombe), Kuruthum Sadik (Chalinze) na Hanan Bafagih (Kisarawe), Mwantum Mgonha (Mkuranga), Shauri Selenda (Bagamoyo), Kassim Ndumbo (Mafia), William Mwakalambile (Nkasi), Lightness Msemo (Sumbawanga), Neema Maghembe (Songea), Sajidu Mohammed (Madaba).

Chiriku Chilumba (Namtumbo), Juma Haji Juma (Mbinga), Nice Munissy (Shinyanga), Halid Mbwana (Bariadi), Veronica Sayore (Busega), Justine Kijazi (Ikungi), John Mgagulwa (Itigi), Asia Mosses (Mkalama), Cecilia Kavishe (Songwe), Regina Beida (Momba), Abdallah Nandonde (Mbozi), Geoffrey Nnaute (Ileje), Shomary Mndolwa (Mji Nzega), Dk Peter Nyanja (Manispaa ya Tabora), Selemani Pandawe (Sikonge), Mariamu Masebu (Mji Handeni) na Halfan Magani (Korogwe).

Wakurugenzi 67 waliohamishwa vituo ni Juma Mhina (Longido-Ngorongoro), Stephen Anderson (Monduli-Longido), Raphale Siumbu (Ngorongoro- Monduli), Athumani Masasi (Chamwino-Bahi), Dk Semistatusa Mashimba Chemba- Chamwino), Lutengano Mwaliba (Magu-Bukombe), Saada Mwaruka (Mafinga- Mbogwe), John Wanga (Ilemela-Geita), Bernard Limbe (Bukoba-Iringa Manispaa) na Innocent Mkandala (Missenyi-Biharamulo).

Hamid Jovu (Iringa-Manispaa ya Bukoba), Fatina Laay (Kasulu-Bukoba), Elias Kayandabila (Mbogwe-Muleba), Waziri Kombo (Biharamulo- Missenyi), Solomon Kamilike (Bukoba-Ngara, Michael Nzyungu (Mpanda- Karagwe), Sacf.

James John (Bariadi-Kyerwa), Ndaki Mhuli (Siha-Kakonko), Upendo Mangali (Kigoma-Siha), Dionis Myinga (Bukombe- Hai), Mwajuma Nasombe (Kilolo-Mwanga) na Dk Rashid Gembe (Mkinga- Moshi Manispaa). Pia Jumla Nnwele (Kibondo-Kilwa), Eston Ngilangwa (Busokelo-Kilwa), John Nchimbi (Babati-Kiteto), Anna Mbogo (Mbulu-Babati), Francis Namaumbo (Makete- Rorya), Palela Nitu (Kalambo- Musoma), Gimbana Ntavyo (Newala Mji- Mji Tarume), Bosco Ndunguru (Manispaa ya Tabora-Manispaa ya Musoma), Solomon Shati (Hanang-Tarime), Changwa Mkwazu (Masasi-Bunda), Kivuma Msangi (Mbarali- Serengeti na Missana Kwangura (Nkasi-Mbarali).

Wamo Tamim Kambona (Kiteto-Chunya), Loema Isaay (Rungwe-Busokelo), Renatus Mchau (Kilwa- Rungwe), Stephen Kaliwa (Kilombero-Mlimba), Kisena Mabuba (Misungwi-Kilosa), Asajile Mwambambale (Kilosa-Gairo), Ally Machela (Tandahimba-Manispaa ya Morogoro), Apoo Tindwa (TarimeVijijini-Masasi), Mussa Gama (Kisarawe-Tandahimba), Modest Apolinary (Geita-Manispaa ya Ilemela) na Lutengano Mwaliba (Magu-Misungwi). Emmanuel Sherembi (Muleba-Ukerewe), Fidelica Myovela (Musoma-Magu), Selemani Sekiete (Nzega-Jiji la Mwanza), William Makufwe (Handeni-Makete), Kenneth Haule Keneth (Handeni Mji-Mji Makambako), Mshamu Munde (Mkuranga- Mji Kibaha), John Kayombo (Musoma-Rufiji), Shafii Mpenda (Madaba-Kalambo), Fredrick Sagamiko (Maswa- Manispaa ya Songea) na Jomary Satura (Lindi-Manispaa ya Shinyanga).

Wamo Simon Berege (Msalala-Maswa), Adrian Jungu (Momba-Mji Bariadi), Msoleni Dakawa (Kondoa- Meatu), Ester Chaula (Ukerewe- Singida), Michael Matomora (Ushetu-Iramba), Oscar Humbe (Bariadi-Manyoni), Zefrin Lubuva (Mwanga-Manispaa ya Singida), Philemon Magesa (Nzega-Mji Tunduma), Kiomoni Kibamba (Jiji la Mwanza-Nzega), Fatuma Latu (Bagamoyo-Igunga) na Sipora Liana (Manispaa ya Kinondoni-Jiji la Tanga).

Wakurugenzi waliobakishwa vituo vyao ni Dk John Pima (Jiji la Arusha), Beatrice Kwai (Manispaa Ubungo), Jumanne Shauri (Jiji la Ilala), Dk Omary Mkulo (Kongwa), Joseph Mafuru (Jiji la Dodoma), Bashir Mhoja (Iringa), Lain Kamendu (Kilolo), Catherine Mashalla (Mpimbwe), Joseph Rwiza (Kasulu), Godwin Chacha (Rombo), Annastazia Buhamvya (Same), Franck Chonya (Ruangwa), Samweli Gunza (Simanjiro) na Ezekiel Magehema (Kyela).

Pia Hassan Njama Hassan (Mvomero), Rehema Bwasi (Morogoro), Emmanuel Mwaigobeko (Manispaa ya Mtwara), Thomas Mwailafu (Mji Nanyamba), Erica Yegella (Mtwara), Duncan Thebas (Newala), Sunday Ndori (Ludewa), Butamo Ndalabwa (Kibaha), Mohamed Mavura (Kibiti), Jacob Mtalitinya (Manispaa ya Sumbawanga) na Jimson Mhagama (Nyasa), Chiza Marando (Tunduru), Grace Quintine (Mji Mbinga) na Anderson Msumba (Mji Kahama).

Wengine ni Emmanuel Matinyi (Kishapu), Elizabeth Gumbo (Itilima), Baraka Zikatimu (Urambo), Hemed Magaro (Uyui), Jerry Mwaga (Kaliua), Gracia Makota (Kilindi), Ikupa Mwasyoge (Lushoto), George Haule (Bumbuli), Isaya Mbenje (Pangani) na Nicodemus John (Korogwe).

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi