loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa aagiza MV Ruvuma, MV Njombe zifanye kazi

Majaliwa aagiza MV Ruvuma, MV Njombe zifanye kazi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha meli za mizigo na abiria za MV Ruvuma na MV Njombe zinaanza kutoa huduma haraka.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa, Majaliwa alitoa maagizo hayo jana alipotembelea Bandari ya Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya na kukuta meli hizo zimeegeshwa.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa, Majaliwa aliagiza TPA ikutane na wafanyabiashara wakubwa na kuzungumza ili kuona namna meli hizo zitakavyosafirisha mizigo nchini na nchi jirani ya Malawi.

“Sisi tuna fursa ya kuwa na maziwa na mafundi wa kampuni zinazotengeneza hata boti, lakini hatuzitumii; kwa hiyo TPA lazima iwe na wabunifu watakaowezesha wananchi kunufaika,” alisema Majaliwa.

Aliongeza: “Meli zimekaa hapo kwa kushindwa kwenda kubeba makaa ya mawe; kwa kushindwa kukubaliana bei; nyie mnataka Sh ngapi na zinapokaa hapo mnapoteza Sh ngapi.” Alisema TPA inapaswa kufanya hesabu kuona gharama za uendeshaji wa kwenda kubeba makaa ya mawe kwa kuanzia na faida ndogo kuliko kuziegesha tu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi