loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mkimbizi akamatwa na AK 47 na risasi 176

Mkimbizi akamatwa na AK 47 na risasi 176

POLISI mkoani Kigoma wamemkamata mtu aliyetambuliwa kuwa ni raia wa Burundi akituhumiwa kuhusika na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika barabara kuu ya Kasulu kwenda Kibondo.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, James Manyama amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Sabushike Abraham maarufu kwa jina la Kayuki (33).

Mtuhumiwa anadaiwa kuwa ni mkimbizi wa Burundi anayehifadhiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya nduta wilayni Kibondo.

Kamanda Manyama alisema mwishoni mwa wiki iliyopita polisi walimkamata mtuhumiwa katika kijiji cha Busunzu wilayani Kibindo akiwa na bunduki aina ya AK 47 yenye magazine mbili zilizokuwa na risasi 176.

Alisema mtuhumiwa alikamaatwa baada ya polisi kupata taarifa na wakaweka mtego.

“Baada ya kukamatwa na kuhojiwa aliwapeleka polisi katika kijiji cha Busunzu eneo la Mlimani wilaya ya kibondo mkoani Kigoma ambako amekuwa akificha bunduki yake baada ya matumizi,”Alisema Kamanda Manyama

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi