loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wasiojulilkana wadaiwa kuhujumu mradi wa bil 500/-

Wasiojulilkana wadaiwa kuhujumu mradi wa bil 500/-

WATU wasiojulikana wanadaiwa kuhujumu mradi wa kimkakati unaojengwa kusafi risha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Kenya.

Msimamizi wa mradi Huo, Mhandisi Lawrence Juae, alisema jana kuwa, mradi huo una urefu wa zaidi ya kilometa 414 kwa upande wa Tanzania.

Alisema watu hao wanahujumu mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 500 kwa kukata vyuma, nyaya na kuondoa bolti na kwenda kuziuza kama vyuma chakavu.

Alidai kuwa, watu hao wamekuwa wakikata vyuma kutoka kwenye minara mikubwa ya umeme na hivyo, kusababisha mkandarasi ashindwe kuendelea na kazi kwa mtiririko aliouweka sanjari na kupata hasara kwani analazimika kununua vifaa ambavyo alikuwa amenunua kabla. Mradi huo unajengwa kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya.

Kwa upande wa Tanzania, mradi huo unajenga kutoka Singida hadi Namanga na kwa Kenya, unajenga kuanzia Namanga hadi Isinya, ukiwa na urefu wa kilometa 510.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndepesi, Losinyati Laizer, alisema hawatakubali kuona watu waaendelea kuhujumu mradi huo.

Kiongozi wa mila, Saito Mollel, alilaani hujuma hizo na kusema kuanzia sasa kila mwananchi atauchukulia mradi huo kama mali yake na kwamba, wataunganisha nguvu kuutunza.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Longido

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi