loader
Dstv Habarileo  Mobile
EXPRESS YAKWEA KILELENI KUNDI A CECAFA

EXPRESS YAKWEA KILELENI KUNDI A CECAFA

TIMU ya Express ya Uganda imeanza vema michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini, ukiwa ni mchezo wa pili wa Kundi A uliochezwa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam jana.

Express ambao ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo, walipata bao hilo pekee dakika ya tano kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na mshambuliaji Erick Kambale baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi wa kati wa Atlabara, Peter Sunday.

Miamba hiyo ya Uganda ililazimika kumaliza dakika 90 ikiwa pungufu baada ya mchezaji wa timu hiyo, Abele Eturude kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 70 kutokana na mchezo usiokuwa wa kiungwana.

Express wanasaka ubingwa wao wa kwanza wa michuano ya Cecafa tangu walipoanza kushiriki mashindano hayo licha ya kucheza fainali mara mbili mwaka 1994 wakafungwa na El Merrick mabao 2-1 na 1995 walipopoteza mbele ya Simba kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.

Ushindi huo umewafanya washindi hao kufikisha pinti tatu na kukaa kileleni mwa kundi lao na kuziacha Yanga na Nyasa zikiwa na pointi moja, huku Atlabara wakiwa hawana pointi hata moja.

Mchezo ujao, Express itajitupa uwanjani Agosti 4 kuwakabili Nyasa Big Bullets, mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b8f0c740354ee4b8492605be98db9ce9.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi