loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ofisi ya Bunge, Kodi inakatwa kama kawa

Ofisi ya Bunge, Kodi inakatwa kama kawa

OFISI ya Bunge la Tanzania imesema, wabunge kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma na viongozi wa kisiasa hivyo wanakatwa kodi zote stahiki kwa mujibu wa sheria.

Miongoni mwa kodi hizo ni kodi ya mapato (PAYE), inayokatwa kwenye mishahara ya wabunge ya kila mwezi.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Uhisiano wa Kimataifa ya Bunge la Tanzania, iliyotolewa leo Jumanne, Agosti 3,  2021, imesema kinachoendelea mitandaoni kwamba wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara hao hakina ukweli.

Ofisi hiyo ya Bunge, imetoa ufafanuzi huo baada ya siku za hivi karibuni, kuibuka taarifa mitandaoni kwamba, wabunge hawalipi kodi hivyo maumivu wanayoyapata  wananchi kupitia tozo za miamala ya simu hawahusiki nayo.

Tozo hizo, zilianza kutumika Julai 15, 2021, baada ya kupitishwa na Bunge. Tozo hizo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kwamba zinawaumiza na tayari Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, ameagiza zipitiwe upya kuangalia kama zinaweza kupunguzwa

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi