loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga kurusha kete nyingine Kagame

Yanga kurusha kete nyingine Kagame

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1:00 usiku, kuikabili Atlabara FC ya Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini.

The Express ya Uganda ndio vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Atlebara bao 1-0, hivyo matokeo hayo yanaifanya Yanga kushika nafasi ya pili kwenye kundi hilo wakiwa na pointi moja sawa na Nyasa Bullets inayoshika nafasi ya tatu na Atlabara inaburuza mkia ikiwa haina pointi.

Kutokana na na matokeo hayo, ni dhahiri kikosi cha Yanga kitaingia kwenye mchezo wa leo kwa lengo la kuondoka na pointi tatu ambazo zitaiweka katika nafasi nzuri ya kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazoingia nusu fainali.

Kocha wa Yanga, Razak Siwa alisema jana kuwa, amerekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita na vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa leo na ana matumaini ya kupata ushindi.

“Mapumziko ya siku mbili yametusaidia kuwarudisha vijana kwenye ubora wao ikilinganishwa na mchezo wa kwanza ambao tulicheza baadhi ya wachezaji wakiwa na uchovu wa safari kama Jimmy Ukonde na Dickson Ambundo ndio maana nina imani tunakwenda kushinda,” alisema Siwa.

Kocha huyo alisema kwa maandalizi waliyofanya wataonesha kandanda la kuvutia ingawa anatambua kuwa mchezo utakuwa na ushindani sababu wapinzani wao Atlabara siyo timu dhaifu.

Ukimtoa kipa Ramadhan Kabwili ambaye hatakuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu, Siwa alisema kikosi chake kitakuwa na mabadiliko kidogo, kipa atamtumia, Geofrey Magaigwa.

Alisema Said Makapu anatarajiwa kuingia kikosini baada ya kukosa mchezo uliopita sambamba na chipukizi Omar Chibada, wakati Wazir Junior na Juma Mahadhi wakianza kama ilivyokuwa mchezo uliopita na viungo wa pembeni amepanga kuwatumia Ambundo na Ukonde.

Mchezo huo utatanguliwa na mechi kati ya Nyasa Bullets dhidi ya vinara wa kundi hilo The Experess mchezo ambao utaanza saa 10: 00 jioni kwenye uwanja huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6ed342b4c37acf7a6f8dcf418b4abcb6.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi