loader
Dstv Habarileo  Mobile
Makambo, Mayele watoa neno Yanga

Makambo, Mayele watoa neno Yanga

WACHEZAJI wapya wa kimataifa wa Yanga, Haritier Makambo na Fiston Mayele wameahidi kupambana kuisaidia timu hiyo kufi kia malengo yaliyokusudiwa ya kutwaa ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Wachezaji hao walitambulishwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa ambaye alisema wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

Kwa upande wa Makambo ambaye anarejea katika timu hiyo akitokea Horoya AC ya Guinea, alisema amefurahi kurudi nyumbani na yuko tayari kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na kuisaidia timu hiyo kuchukua makombe msimu ujao.

“Asante sana nafurahi kurudi nyumbani, ni Makambo yule wanayemjua amerudi. Natumaini tutafanya kazi kama tuliyokuwa tunafanya kila siku, kurejesha furaha na mataji,” alisema.

Makambo aliyewahi kuitumikia Yanga msimu wa mwaka 2018/2019 alisema: “Unajua Yanga ni timu kubwa ina malengo ya kutaka kuchukua ubingwa kila mwaka, tutapambana kufikia malengo hayo.”

Kwa upande wake, Mayele anayotokea AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo alisema amefurahi kujiunga na timu hiyo na kuahidi kufanya jitihada kubwa na kutimiza malengo yaliyowekwa na klabu.

Mfikirwa alisema usajili bado unaendelea hivyo wana Yanga watarajie mambo mazuri zaidi yanayokuja.

“Safari bado inaendelea kwa kasi wana Yanga watarajie mambo mazuri, tunaendelea kujenga timu yetu na ujenzi wa timu sio wa siku moja,” alisema.

Alisema wamefanya tathmini ya kutosha na kujiridhisha kuwa wachezaji waliosajiliwa ni watu sahihi katika timu hiyo.

“Ukiangalia rekodi kwa mfano za Mayele sio mbaya, alikuwa akifanya vizuri AS Vita, mwalimu ameona ni mchezaji anayetufaa kwa sababu pia ana uzoefu na michezo ya kimataifa,” alisema.

Mbali na hao, mwingine ambaye tayari ametambulishwa ni Yusuph Athuman kutoka Gwambina.

Kuna wengine hawajatambulishwa rasmi lakini walionekana wakiwa wamevaa jezi za Yanga katika michuano ya Cecafa Yanga ilopocheza na Big Bullets ni Dikson Ambundo kutoka Dodoma Jiji na Jimmy Julio kutoka UD Songo ya Msumbiji.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a5ed502d0712aedb2197e9aa69765cb3.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi