loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mnaotarajia kustaafu tumieni vyema fedha’

Mnaotarajia kustaafu tumieni vyema fedha’

VIONGOZI waandamizi wa benki ya NBC Morogoro, Mtwara na Zanzibar, wamewashauri watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi kuweka mikakati thabiti ya matumizi bora ya fedha sambamba na kupata elimu sahihi kuhusu huduma za kifedha na uwekezaji wa miradi sahihi, ili wanufaike hasa baada ya kustaafu.

Walitoa mwito huo walipozungumza na wastaafu watarajiwa katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo.

Akizungumza kwenye moja ya semina hizo mkoani Morogoro, Meneja Mikopo kutoka Benki ya NBC, Mtenya Cheya, aliwataka watumishi hao kuheshimu na kutunza fedha zao katika taasisi zinazoaminika na kubuni vyanzo vya mapato kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalamu.

“NBC tumejipanga kuwasaidia wastaafu watarajiwa na wale waliokwishastaafu na ndio sababu pamoja na kushiriki kwenye semina za mafunzo kama hizi, pia tumekuwa na mikakati na huduma bora kwa wastaafu zikiwemo za kutoa mikopo inayozingatia mahitaji yao,” alisema.

Akizungumza katika semina kama hiyo mkoani Mtwara, Meneja wa NMB, Tawi la Mtwara, Emmanuel Mseti, aliwataka wastaafu hao watarajiwa kuhakikisha wanawashirikisha wataalamu wa fedha wanapofikiria kuhusu mawazo ya biashara, uwekezaji na matumizi sahihi ya mikopo yao ili kujihakikishia ufanisi wa matumizi ya mafao yao.

“Ndio maana benki ya NBC tumekuwa na utaratibu mzuri wa kuwapatia mafunzo wateja wetu kupitia mipango mbalimbali ukiwemo mpango wa klabu za biashara na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwajengea uwezo wateja wetu wa kufanya biashara kabla hatujawajakopesha,” alisema.

Wito kama huo pia ulitolewa Zanzibar na Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Abel Kaseko aliyewataka wastaafu na wastaafu watarajiwa kuhakikisha wanahifadhi fedha zao kwenye taasisi rasmi za kifedha kama benki ya NBC ili kuepuka matapeli.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1ae0a04bf5f74f81d46692d8d8c98eca.jpg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi