loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dar ya kwanza saluni inayotembea

Dar ya kwanza saluni inayotembea

Dar es Salaam imetajwa kuwa mkoa wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma ya Saluni inayotembea lengo likiwa ni kusogeza huduma  karibu zaidi na wananchi.

Mtaalam Mwelekezi, Haris Kapiga, ameyasema hayo jana Agosti 4, 2021 wakati akizindua gari maalum ambalo ndio saluni inayotembea.

“Kwa kuwa Dar es Salaam ni Mkoa wa kwanza Tanzania katika kuanzisha huduma hii ni vyema mkatoa huduma bora zenye viwango ili mikoa mingine ivutiwe na kuja kujifunza kutoka kwenu,” alisema Kapiga na kuongeza

“Kila mtu anafanya biashara lakini kila mtu anafahamu namna ya kuwafikia wateja wake, J & R watafikia wateja makazini, watawasuka, kunyoa ndevu na huduma nyingine zote zitolewazo na saluni, wamekuja kutofautisha tupo kwenye soko la ushindani, wanakufuata ulipo,” alisema Kapiga

Aidha; Kapiga aliwataka aliwataka watumishi wa hao kufanya kazi kwa ushirikiano ‘team work’ kwa kuwa ndio nguzo kuu ya mafanikio.

“Nawaomba kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta matokeo chanya ya huduma hii,” alisema

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/155bef2b718ada438ecb3a96dd05ad6c.jpg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi