loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wauzaji simu kicheko, kuondolewa kodi kwenye simu janja

Wauzaji simu kicheko, kuondolewa kodi kwenye simu janja

WAKATI serikali ikisamehe kodi kwenye simu janga, vishikwambi na modemu, lengo likiwa kufikia asilimia 80 kutoka asilimia 46 iliyopo sasa ya watumiaji wa intaneti ifikapo 2025, Kampuni ya simu ya Oppo  na Samsung wamesema kuondolewa kwa Kodi (VAT) kumeongeza  wigo wa matumizi ya simu hizo kwa watanzania.

Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 limeondoa kodi ya asilimia 18 kwenye simu janja ili kila mwananchi  aweze kutumia simu hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Usambazaji wa Bidhaa za kampuni ya Oppo, Mbwana Mpeta, amesema serikali imefanya jambo kubwa sana kwa kuondoa kodi katika simu janja ili kila mtanzania aweze kumiliki.

Amesema, wao kama kampuni ya Oppo wamejipanga kuweza kuhakikisha simu zao zinakuwa katika bei nafuu na kila mwananchi anapata fursa ya kumiliki simu janja na kuwa katika ulimwengu wa Kidijitali.

“Dunia imekuja ni kijiji, leo Oppo na Samsung tumezindua kwa pamoja duka hili katika jengo la China Plaza ukifika utapata simu aina zote na kwa bei  nzuri lakini kikubwa ni kuondolewa kwa VAT hii inapelekea kwa sisi makampuni kupunguza bei za simu janja ili wananchi hadi wa kipato cha chini waweze kumiliki,”amesema

Naye Meneja Bidhaa wa Samsung, Julius Giabe amesema kwa sasa kuna soko kubwa la ushindani ila  kwa upande wao wamejipanga kuleta bidhaa zenye ubora na uwezo mkubwa.

Ameishukuru serikali kwa kuondoa kodi (VAT) kwa simu janja na hiyo ni chachu ya kufanikisha Tanzania katika dunia ya kidijitali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6886c61a7b2879853977dc64fc3b1236.jpg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi