loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tutofautishe demokrasia na fujo za kisiasa

Tutofautishe demokrasia na fujo za kisiasa

TANZANIA ni nchi yenye vyama vingi vya siasa. Miongoni mwa vyama hivyo, ni chama tawala yaani Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na chama cha NCCR-Mageuzi.

 

Vingine miongoni mwa vingi, ni ACT-Wazalendo, Alliance for Democratic Change (ADC), Sauti ya Umma, Ada- Tadea, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma) na Tanzania Labour Party (TLP).

 

Kimsingi, vyama hivi na vingine ambavyo sikuvitaja vipo na vinaendesha shughuli zao kama kawaida kupitia mfumo huu ulioanza nchini mwaka 1992.

 

Ninawapongeza Watanzania wote wanaotumia fursa ya mfumo wa vyama vingi nchini, kuendesha siasa za kistaarabu zinazolenga na kuchochea hasa maendeleo, huku zikiweka kando vurugu.

 

Hao ndio miongoni mwao licha ya kuwa walikuwa na upinzani na wengine hata ni viongozi katika vyama vya upinzani, bado serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetambua mchango wao katika maendeleo ya taifa na kudumisha amani kiasi cha kuwateua katika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini.

 

Mfano ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kustaafu na kufariki dunia hivi karibuni, Dk Anna Mghwira. Huyu alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo.

 

Mwingine ni aliyekuwa Mgombea Urais kupitia ADC, Queen Sendiga ambaye Rais Samia Suluhu amemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. 

 

Kimsingi, wapo wanasiasa wengi wa upinzani ambao ni makini na wanaoonesha uzalendo katika nchi yao wakidhihirisha kuwa, upinzani si kupinga kila kitu hata cha manufaa kwa taifa wala kutaka kusababisha vurugu kila mara.

 

Ndio maana juzi wakati akizungumza katika kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Rais Samia alisema Tanzania ina demokrasia ya kisiasa na akawataka Watanzania watofautishe demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa.

 

Nionavyo mimi, wanasiasa wengi wa upinzani nchini, wanafanya vurugu za kisiasa na siyo  demokrasia ya kisiasa. Hao, kwa malengo yao binafsi, wanajificha katika mgongo wa demokrasia ili kuchochea vurugu nchini.

 

Hao, ili waone kuna demokrasia ya siasa, ni lazima mambo mawili makubwa yafanyike. Kwanza, hata kama hawakushinda katika uchaguzi, wanataka watangazwe kuwa wameshinda.

 

Lingine ambalo likifanyika watasema wameiona demokrasia ya kisiasa, ni pale watakapoachiwa wafanye lolote, mahali popote, wakati wowote na kwa njia yoyote tena dhidi ya yeyote yaani, wafanye vurugu za kisiasa; hapo, watasema wanaiona demokrasia ya siasa nchini.

 

Hili la vurugu za kisiasa kama njia ya demokrasia ya kisiasa, ni jambo lisilokubalika wala kuvumiliwa maana watu wanataka siasa za kistaarabu na si kujificha katika siasa ili kufanya vurugu.

Ndio maana ninasema: “Tutofautishe demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/868a06514585022f0da8bc747682d1d9.jpeg

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi