loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga: Usajili wetu umejitosheleza

Yanga: Usajili wetu umejitosheleza

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Dominic Albinus amesema kwa sasa wamejitosheleza kwenye usajili wao, kilichobaki ni kuingia kwenye mashindano.

Alisema wanaamini watafanya vizuri msimu wa mwaka 2021/ 22, kwa sababu wachezaji wote iliowasajili ni kwa matakwa ya kocha wao, Nasreddine Nabi.

Shirikisho la Soka Tanzania, TFF hivi karibuni lilitangaza klabu zinaruhusiwa kusajili wachezaji 12 wa kigeni, ikiruhusiwa kutumia wanane kwa mechi moja ya mashindano ya ndani.

Awali, klabu ziliruhusiwa kusajili wachezaji 10 na kuwatumia wote kwenye mechi moja. 

Akizungumza na gazeti hili jana, Albinus alikiri kufurahishwa na mapendekezo hayo lakini akasema kwa sasa hawana mpango wa kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni labda kwenye dirisha dogo endapo kocha wao atabaini mapungufu na atahitaji kuongeza mchezaji.

“Yanga tuna imani kubwa na usajili ambao tumeufanya, namaanisha wachezaji wazawa na hata wa kigeni, mapendekezo ya Rais Karia tumeyasikia lakini kwa sasa tumeona tufanye kazi kwanza na hawa ambao tumewasajili huko mbele kama kocha atahitaji mtu tunamwongezea,” alisema.

Kiongozi huyo alisema pamoja na msimu huu kukabiliwa na mashindano mengi, hawana shaka na wachezaji waliowasajili wakiamini wana uwezo wa kupambana na kuipa Yanga mafanikio.

Albinus alisema, baada ya kukamilisha usajili wamemkabidhi kocha Nabi  kila kitu ikiwemo uwajibikaji wa wachezaji pamoja na viwango vyao endapo kutatokea mapungufu yoyote yeye ndiye atautaarifu uongozi na kuwapa mapendekezo yake kwamba anahitaji mchezaji wa aina gani na wao watamletea.

Alisema kwa kazi waliyofanya kwenye usajili, anaamini hakuna kitakachowasumbua. 

Yanga imesajili wachezaji saba wa kigeni ambao ni Kipa Djigui Diarra kutoka Mali, Fiston Mayele, Jesus Moloko, Heritier Makambo, Yannick Bangala na Djuma Shabani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Khalid Aucho kutoka Uganda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/490223c7d250b063b9b2e0c85c1af130.png

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi