loader
Dstv Habarileo  Mobile
Matola ammwagia sifa beki mpya

Matola ammwagia sifa beki mpya

KOCHA msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amemmwagia sifa beki mpya wa timu hiyo, Henock Inonga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akisema ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chao cha msimu wa mwaka 2021/22.

Beki huyo amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea DC Motemapembe ya Congo kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza na gazeti hili kutokea Morocco walipoweka kambi, Matola alisema siku walizofanya mazoezi beki huyo ameonesha utofauti mkubwa ikiwemo namna ya kuwadhibiti washambuliaji hatari na kuanzisha mashambulizi.

“Huyu Inonga tumepata mtu hapa, anasifa zote ambazo beki anatakiwa kuwa nazo anajua kukaba, anapiga vichwa lakini kitu kizuri yupo vizuri kwenye kuanzisha mashambulizi ngoja tusubiri ligi ianze watu watajionea wenyewe,” alisema Matola.

Aidha, Matola alisema bado wanaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa na wakiwa Morocco, wanafanya mazoezi mbalimbali ikiwemo kujenga misuli kwenye gym, kimbinu na mifumo ya kutumia vitu ambavyo ndio muhimu katika kipindi hiki cha maandalizi.

Alisema uwajibikaji wa wachezaji wote ikiwemo wale wageni unakwenda vizuri na wanatarajiwa kuwa na kikosi bora pengine kuliko hata kile cha misimu miwili iliyopita ambayo walifanya vizuri na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Inonga anatajwa kutua Simba kusaidiana na mkongwe Pascal Wawa, ambaye licha ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja lakini ameonesha kuchoka kitu kinachomshinda kuendana na kasi ya wachezaji chipukizi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7e1fd111f158dc0b9f03961c4565a250.jpeg

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi