loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shime atamba kung’ara Cecafa

Shime atamba kung’ara Cecafa

KOCHA wa timu za soka za taifa za wanawake, Bakari Shime amesema anaamini mchezo wa kwanza wa mashindano ya Cosafa dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa Septemba 16 ni mwanzo mzuri wa kutwaa taji hilo.

Mashindano ya Cosafa yatafanyika kwenye mji wa Nelson Mandela Bay, Afrika Kusini kuanzia Septemba 15-26 na Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Zimbabwe, Botswana na Sudan Kusini.

 Shime anaamini mashindano hayo yatakuwa maandalizi mazuri ya kujiandaa na Afcon.

“Naamini utakuwa mchezo wenye ushindani kwani katika mashindano yaliyopita tuliwafunga, hivyo watahitaji kulipa kisasi wakati sisi tutakuwa tunataka kuendeleza ubabe,” alisema Shime.

Shime alisema kushinda mchezo wa awali itasaidia kujiamini katika michezo inayofuata, ambapo Septemba 19 watacheza na Botswana ambao katika mashindano yaliyopita waliifunga Tanzania na mchezo wa mwisho katika makundi watacheza na Sudan Kusini Septemba 21.

Katika mashindano yaliyopita, Twiga ilitolewa katika hatua ya makundi huku U-17 wakichukua ubingwa kwa kuifunga Zambia, hivyo safari hii wana kibarua cha kwenda kulipa kisasi.

Tanzania, Sudan Kusini na Uganda ni timu tatu kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) zitakazoshiriki katika mashindano hayo. 

Mashindano hayo, yatazihushisha timu 12 pamoja na mabingwa watetezi Banyana Banyana kutoka Afrika Kusini na Zambia ambao wametoka kwenye Michezo ya Olimpiki.

Kundi A: Afrika Kusini, Angola, Malawi na Msumbiji, Kundi B lina Botswana, Tanzania, Sudan Kusini na Zimbabwe na Kundi C ni Zambia, Namibia, eSwatini na Uganda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1e959f7cd4cc25fc8ce6e1d596b8ad42.jpeg

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi