loader
Dstv Habarileo  Mobile
Miquissone Aaga Rasmi Simba

Miquissone Aaga Rasmi Simba

Nyota Raia wa Msumbiji Luis MIquissone alie kuwa akikipiga katika klabu ya Simba  ameaga rasmi na kuwashukuru mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram .

Kupitia ukurasa wake rasmi Luis ameandika”Wapendwa Familia ya Simba asanteni kwa kunipenda na kunifanya mmoja wenu”

“Shukrani za dhati ni kwa Bodi, Mwenyekiti, Mkurugenzi Mkuu, Menejimenti, wafanyakazi pamoja na wachezaji wenzangu wote mabingwa”

“Nawezaje kusahau mashabiki mtaendelea kubaki kwenye moyo wangu.

“Haukuwa uwamuzi rahisi kuondoka Simba lakini ilinibidi kutafuta changamoto nyingine, mpaka tutakapo onana tena”.

Luis ambae alisajiliwa msimu wa 2019/20 kutokea klabu ya UD songo ya Msumbiji ameisaidia Simba  kushinda ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara Mara mbili mfululizo pamoja na Azam sports Federation cup (ASFC) mara mbili mfululizo na kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Africa.

Ikumbukwe Simba  walithibitisha  kumuuza mchezaji huyo ingawa haikutajwa rasmi anaelekea timu ipi na kwa dau la kiasi gani ingawa tetesi zinasema kuwa amesajiliwa na miamba ya Misri Al Ahly Sc  .

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d54fe365663ec4c70c336d791367f158.jpg

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Robinson shoo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi