loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kabwili arejeshwa Stars, 28 kujiandaa Kombe la Dunia

Kabwili arejeshwa Stars, 28 kujiandaa Kombe la Dunia

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen,  amemrejesha kikosini kipa Ramadhani Kabwili wa Yanga katika kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini Agosti 24 kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia, 2022 Qatar

Taifa Stars itamenyana na DRC Septemba 2, uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kurejea Dar es Salaam  Septemba 7 kumenyana na Madagascar na Oktoba 10 itaifuata Benin kukamailisha mechi za mzunguko wa kwanza wa kundi lake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Poulsen alisema , “Tumefanya  uchaguzi kwa kuangalia uwezo wa wachezaji kiujumla kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliomalizika hivi karibuni, pia michuano ya CECAFA U23 yaliofanyika nchini Ethiopia na timu ya vijana ya Tanzania kuibuka mabingwa”

Akisisitiza amesema  “Tumechagua wachezaji 28 kuingia kambini kuaza maandalizi ingawa tutasafiri na wachezaji 23 na kuwaacha wachezaji tano ambao ndio namba inayo hitajika kwa sasa tumewaita wote kutokana na dharura mbali mbali zinazoweza kujitokeza ikiwemo majeruhi”.

Alikitaja kikosi cha Taifa Stars kitakacho ingia kambini ni Magolikipa Aishi manuala (Simba Sc),Metacha mnata(mchezaji huru), Ramadhani kabwili (Yanga), Wilbol Maseke (Azam FC), Walinzi ni Shomari Kapombe (Simba Sc)

Erasto Nyoni, Israel Patrick mwenda (Simba Sc) , Dickson Job, Bakari mwamnyeto (Yanga) Kennedy Juma (Simba Sc)

Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Abdulrazack Mohammed (Azam FC), Mohammed Hussein  (Simba Sc), Nickson Kibabage(Youssoufia FC Morocco).

Kwa upande wa viungo ni  Eduward Manyama (Azam FC), Ayoub Lyanga (Azam FC), Meshack Mwamita(Gwambina FC)

Novatus Dismas(Maccabi Tel Aviv -Israel), Mzamiru Yassin (Simba Sc), Mdathir Yahya (Azam FC), Feisal Salum(Yanga) Salum Abubakar(Azam FC), Zawadi Mauya (Yanga) Iddy Selemani(Azam FC) Abdul Hamis Suleiman (Coastal Union)

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Fenerbahce- Uturuki), John Bocco (Simba Sc) na Saimon Msuva(Wydad AC – Morocco).

 

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d87bd4b754c18282e249f06dd8b7f932.jpg

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Robinson shoo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi