loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nabi hataki mzaha Yanga

Nabi hataki mzaha Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewataka wachezaji wake kuweka mbele nidhamu na atakaye kwenda kinyume, adhabu yake ni kukatwa dola za Marekani 100 kwenye mshahara wake ambao ni sawa na Sh 230, 000 za Tanzania.

Kocha huyo aliichukua Yanga mwishoni mwa msimu uliopita akichukua nafasi ya Cedric Kaze, moja ya kitu ambacho hakufurahishwa nacho ilikuwa ni tatizo la nidhamu kwa wachezaji, jambo lililo sababisha mara kadhaa kuwasimamisha baadhi ya wachezaji.

Wachezaji waliokutana na makali ya kocha huyo ni pamoja na Metacha Mnata na mshambuliaji Michael Sarpong ambao ambao kwa sasa wote wametemwa.

Akizungumza na gazeti hili kupitia mtandao wa Facebook jana, Meneja Yanga, Hafidhi Salehe alisema, Nabi aliyasema hayo katika mazoezi ya kikosi hicho katika jiji la Marrakesh, nchini Morocco jana asubuhi.

Alisema hatakuwa tayari kumfumbia macho mchezaji yeyote ambaye hatakwenda sambamba na maagizi yake.

“Kocha alisema hataki kuona wachezaji wake wakipata kadi zisizo kuwa za lazima uwanjani, lakini pia atakuwa mkali kwa wachezaji wanaochelewa kambini na mambo mengine ya kinidhamu atakuwa mkali na hatotaka masihara katika hilo, lengo lake ni kutaka kujenga nidhamu na umoja ndani ya timu,” alisema Hafidhi.

Aidha, kocha huyo raia wa Tunisia alisema kuanzia jana timu yake itakuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, lengo ni kutaka kuendana na muda ambao watakuwa nchini Morocco ili kukamilisha programu yake ambayo aliiandaa kwa kukiweka sawa kikosi chake kabla kuanza kwa mashindano.

Alisema mazoezi ya asubuhi yatakuwa yakianza saa 1:00 na kumalizika saa 5:00 wakati mazoezi ya jioni yatakuwa yakianza saa 1:00 na kumalizika saa 3:00 usiku akisema kwa kufanya hivyo anaamini ataweza kufukuzana na muda ambao ni mfupi kulingana na aina ya programu za kuiandaa timu hiyo.

“Unajua muda ni mdogo alafu kuna baadhi ya wachezaji walioitwa timu ya taifa wataondoka kwa hiyo analazimika kufanya awamu mbili za mazoezi kwa siku ili angalau kila mchezaji aweze kupata vitu muhimu ikiwamo mifumo ambayo watakuwa wakiitumia,” alisema Hafidhi.

Leo ni siku ya nne tangu Yanga ilipotua katika mji wa Marrekesh kupiga kambi hiyo na kwa mujibu wa taarifa za uongozi wa timu hiyo, zimebaki siku sita kabla kufikisha siku 10, ambapo ndio itakuwa mwisho wa kambi hiyo na timu kuanza safari ya kurudi nyumbani kuendelea na ratiba nyingine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2bc7c1bad2154e74e34e2d2e66b38ec6.jpeg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi