loader
Dstv Habarileo  Mobile
Gaguti ataka Bandari Mtwara kuwa wabunifu

Gaguti ataka Bandari Mtwara kuwa wabunifu

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Brigadia Jeneral Marco Gaguti amewataka mamlaka ya Bandari Mtwara kuwa wabunifu katika kuendeleza na kuzalisha fursa za uchumi na biashara pamoja na ajira katika Bandari ya Mtwara ambayo kwa sasa imundombinu yake imeboreshwa na kuwa tayari kwa kuhudumia biashara za usafirishaji.

Gaguti ametoa maagizo hayo jana wakati akifungua mkutano wa wadau wa bandari ya Mtwara ambacho kililenga kuhakikisha Kamba ufanisi wa bandari hiyo unakuwa kwa asilimia 100.

Pia ametaka mamlaka hiyo kuanza kufanya maandalizi ya msingi ya kuhakikisha bandari hiyo inasafirisha korosho zote zitakazovunwa mikoa ya kusini ifikapo mwezi wa kumi mwaka huu na kwamba wasisubiri mpaka mwezi huo ndio waanze kujiandaa.

“Kama serikali ilivyoelekeza kwamba korosho zipitie bandarin hapa kuanzia mwezi wa kumi, tusisubiri mpaka mwezi wa kumi ikakuta kwamba hatuko tayari, muanze kufanya maandalizi ya msingi ifikapo mwezi wa kumi bandari ya Mtwara ifanya kazi iliyokusudiwa kusafirisha korosho,” amesema.

Gaguti pia amewaomba wadau wa bandari kuunga mkono juhudi za serikali ambazo zimelenga kufungua fursa za kiuchumi nyingi za kibiashara nchini na nchi jiran za Comoro, Msumbiji na Malawi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d93d07be4f7871e677998f58ed285173.jpeg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: Na Anne Robbi, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi