loader
Chama aaga Simba

Chama aaga Simba

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Cletus Chama amewaaga wanachama na mashabiki wa klabu hiyo baada ya mchakato wa usajili wake wa kujiunga na klabu ya RS Berkane ya Morocco kukamilika.

Tangu uongozi wa Simba kutoa taarifa za kukamilika kwa dili hilo, mchezaji huyo alikuwa kimya hakusema chochote mpaka jana kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram alipofunguka kwa mara ya kwanza kuzungumzia maumivu yake kwa wanamsimbazi.

Katika taarifa hiyo, Chama alisema ukimya wake ulitokana na kusubiri baadhi ya taratibu za usajili kukamilika, lakini kadri siku zinavyokwenda anaona muda siyo rafiki kwake na hawezi kuendelea kukaa kimya bila kutoa shukrani zake kwa mashabiki wa Simba.

Chama alisema wakati anatua Dar es Salaam mwaka 2018, au kupata nafasi ya kuipa furaha mioyo yao kupitia kipaji chake cha soka, lakini ilikuwa tofauti na mawazo yake kwani mapenzi aliyopata kwa muda wote alioishi Tanzania ni ya hali ya juu na hakutegemea kama ingekuwa hivyo, na atayathamini kwa maisha yake yote.

“Siwezi kuelezea jinsi ninavyo ipenda Simba, kutokana na mapenzi makubwa na ushirikiano ambao nimeoneshwa mambo mengi yatabaki kwenye kumbukumbu yangu ingawa bado siamini kwamba jina langu halitotangazwa tena na Baraka Mpenja msimu ujao, au kuvaa jezi namba 17 kwa timu niliyoipenda,” alisema Chama.

Aidha, mchezaji huyo aliwashukuru viongozi wa timu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji, ‘MO’ na Mkurugenzi Mtendaji, Barbra Gonzalez, wasimamizi wa klabu, benchi la ufundi na wachezaji wenzake wapendwa, akisema anajisikia heshima kufanya nao kazi.

Chama alisema anaondoka Simba akiwa hajutii kwa jasho ambalo amelitoa na mafanikio aliyoipa timu hiyo na uongozi kumtimizia mahitaji yake muhimu kama mwajiriwa wake, hivyo anakwenda kuanza maisha mapya na hivyo ndivyo yalivyo maisha ya mchezaji, hajui msimu ujao atakuwa wapi, hivyo angeomba wamwombee mafanikio huko aliko.

“Nawashukuru viongozi wangu wa Simba kwa busara zao walizotumia wakati 

wa majadiliano kuhusu usajili wangu na timu yangu mpya nawashukuru kwa kunikubalia kuondoka lakini pia siwezi kuwasahau mashabiki wangu wapenzi, mmekuwa watu muhimu katika maisha yangu ndani ya Simba,”alisema Chama.

Alisema pamoja na kwamba ameondoka Simba lakini ataendelea kuwa shabiki wa timu hiyo katika hali yoyote jua na mvua, ingawa atalazimika kuwa mpinzani wao watakapokutana kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati huo huo, uongozi wa klabu ya Simba jana ulimtambulisha kiungo mkabaji Sadio Kanoute raia wa Mali aliyesaini mkata wa miaka miwili akitokea timu ya Al Ahly Tripoli ya Libya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f2539b4f12a9509725be600f55b19a46.jpeg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi