loader
Bashungwa awataka wazazi kuendeleza vipaji vya watoto

Bashungwa awataka wazazi kuendeleza vipaji vya watoto

WAZAZI wametakiwa kuwekeza katika kuendeleza vipawa vya watoto wao sambamba na masomo yao.

Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, baada ya majumuisho ya safari yake

ya kutembelea timu za taifa za soka za wanawake za Twiga Stars, Tanzanite na timu ya taifa ya mpira wa wavu Dar es Salaam jana.

Alisema, jitihada ambazo wazazi wanaweka katika kuwasukuma watoto katika masomo, jitihada hizo hizo ziwekwe kumsukuma katika michezo.

“Watoto wanazaliwa na vipawa vya michezo, sanaa na vinginevyo kwa hiyo ni vizuri tukaviendeleza vyote kwa sababu hujui Mwenyezi Mungu kampangia nini,” alisema Bashungwa huku akimtolea mfano mchezaji wa Twiga Stars, Janeth Christopher, ambaye anasoma shahada Chuo cha Uhasibu (TIA).

Alisema, Janeth ni kielelezo kwa wazazi kuwa watoto wanaweza kuwa na mafanikio mbalimbali, kwani licha ya kucheza soka, kidato cha nne alifaulu kwa daraja la kwanza na kidato cha sita vivyo hivyo.

Pia alitolea mfano kuwa, matajiri wengi duniani ni wana michezo na wasanii.

Alisema serikali itaendelea kuzisaidia timu za taifa na hakuna timu itakayoshindwa

kusafiri kwa sababu serikali imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ambao asilimia tano ya mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha itakuwa inaingia huko.

Aidha, Bashungwa aliwataka wanamichezo na viongozi wa michezo kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya virusi vya corona kwa sababu

mtu ambaye amepata chanjo hiyo akipata ugonjwa wa covid-19 ni rahisi kupona kuliko ambaye hana chanjo.

Aliwataka wote ambao hawajachanja kwenda Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kupata chanjo leo kwani huduma hiyo itakuwa inatolewa bure na serikali kwa kushirikiana na Wilaya ya Temeke.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/21f5cf3364ca949cbcad046a1ca2c125.jpeg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi