loader
Makusanyo ya kodi yafikiayafikia asilimia 97

Makusanyo ya kodi yafikiayafikia asilimia 97

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh trilioni 1.535 mwezi uliopita ikiwa ni sawa na asilimia 97.4 ya malengo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ukusanyaji wa mapato unaendelea kuimarika.

“Kiasi hiki ni kikubwa ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi Julai mwaka jana ambapo ilikusanya Sh trilioni 1.284 sawa na asilimia 84.1 ya lengo. Ukusanyaji huu hauhusiani na tozo za miamala ya simu,” alisema.

Aliwapongeza Watanzania kwa kuitikia kulipa kodi bila shuruti na akasisitiza kuwa, serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uzalishaji na ufanyaji biashara ili kodi iongezezeke kwa ajili ya kwenda kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alihimiza wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi kwa kuwa kodi ni kwa manufaa yao na taifa kwa jumla kupitia huduma mbalimbali za kijamii na miradi ya maendeleo.

“Fedha zinazokusanywa haziendi kwenye mfuko wa mtu binafsi, bali zinakwenda kutekeleza miradi ya maendeleo, unapolipa kodi unajenga barabara, kituo cha afya unapeleka maji na huduma nyingine. Watanzania tujisikie fahari kulipa kodi,” alisema.

Tozo za miamala

Kuhusu tozo za miamala, Msigwa alisema keshokutwa serikali itatoa taarifa rasmi ya uamuzi wake kwa suala hilo na namna tozo hizo zitakavyowekwa.

“Kulikuwa na maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuangalia viwango vya tozo. Niwahakikishie Watanzania kuwa, kazi inafanyika. Kodi iko kwa sheria ya Bunge, hivyo kuna kazi ya kiuangalifu inafanyika  ili sheria isivunjwe,” alisema.

Akafafanua: “Tayari Kamati iliyoundwa imeshafanya kazi na imewasilisha taarifa ya kwanza kwa Waziri Mkuu ambaye ameagiza marekebisho zaidi yakafanyike na sasa taarifa rasmi ya nini serikali imeamua itatolewa tarehe 31 mwezi huu.”

Msigwa alisema tozo ya miamala ni ya mshikamano ambayo serikali imeiazisha kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa miradi na huduma kwa wananchi.

Wakati huo huo: Msigwa amesema Julai mwaka huu, TRA imeanza kukusanya kodi ya majengo kupitia mita za umeme maarufu Luku na kuwa, malengo ni kukusanya Sh bilioni 46.517 kwa mwaka huu 2021/22.

Alisema kwa kuwa utaratibu huo ni mpya, TRA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wanafanyia kazi baadhi ya changamoto ikiwemo kuwataka wamiliki wa nyumba kujitokeza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/218a776eec616e77fbbbd944ebc5c968.jpeg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi