loader
Senzo CEO Yanga

Senzo CEO Yanga

UONGOZI  wa klabu ya Yanga umemtangaza Senzo Mbatha kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo.

Senzo amepewa nafasi hiyo ukiwa ni utekelezwaji wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Raia huyo wa Afrika Kusini aliyekuwa mshauri wa masuala ya mabadiliko wa klabu hiyo, amepewa nafasi hiyo kutokana na juhudi kubwa alizofanya kujenga miongozo mizuri ya mabadiliko hayo ambayo wamepania kuitekeleza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,  Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa anarudi kwenye nafasi yake ya awali ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

“Nichukue nafasi hii kumpongeza Mfikirwa kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi kifupi kana kwamba alishawahi kuongoza klabu kubwa kama Yanga, ingawa bado ataendelea kutoa ushirikiano kwa waandishi endapo mtahitaji msaada wake,” alisema Mwakalebela.

Kwa upande wake, Senzo aliushukuru uongozi wa Yanga kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo kubwa ya kubadilisha mifumo na miundombinu ya kuiendesha klabu hiyo na kuifanya kuwa ya kisasa kama zilivyo klabu nyingine kubwa duniani.

Senzo aliyewahi kuhudumu Simba katika nafasi ya Mtendaji Mkuu, alisema yupo tayari kukabiliana na changamoto zote kuhakikisha Yanga inatekeleza ipasavyo yale yote iliyoahidi.

“Uongozi na wanachama na mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu, nipo tayari kukabiliana na changamoto zote kuhusiana na mambo ya mabadiliko, kitu cha msingi hapa ni lazima tufikie lengo kama tulivyowaahidi wanachama na mashabiki wetu wakati tunataka kuingia kwenye mfumo huu nitashirikiana na La Liga na wote wanaohusika ili Yanga iweze kuwa bora Afrika,” alisema Senzo.

Naye Mfikirwa aliwashukuru waandishi wa habari kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote ambacho alikaimu nafasi ya Katibu Mkuu na kuwataka wampe ushirikiano Senzo. 

Alisema kwa muda aliofanya naye kazi, amebaini ni mtendaji wa kweli mwenye kuipenda kazi yake hivyo itakuwa vizuri kumpa ushirikiano ili  kuyajua mengi mazuri ambayo Yanga wamekusudia kuyafanya katika mpango wao wa kuifanya timu hiyo kufanya vizuri kuanzia msimu unaokuja.

Aidha, Mwakalebela aliwapongeza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi na kuwapa sapoti kubwa wachezaji pamoja na wadhamini wao wote ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha shughuli yao.

Alisema pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Zanaco, timu hiyo ipo kambini Avic Town Kigamboni ikiendelea na maandalizi ya msimu ujao na wanampango wa kumpatia kocha wao mechi nyingine za kirafiki ili kukiweka sawa kikosi hicho kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria Septemba 12.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/10d5a33d2ffeaf2274f0e184ae1fac2b.jpeg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi