loader
Stars kuikabili Congo leo

Stars kuikabili Congo leo

TIMU yaTaifaya Tanzania ‘Taifa Stars’     leo inashuka uwanjani kumenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kwanza wakuwania nafasi yakufuzu fainali za Kombe la Dunia katika Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi.

Stars inashuka katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Congo, ambapo mara ya mwisho walipokutana Agosti 27,2018 katika mchezo wa kirafiki Dar es Salaam, Stars ilishinda2-0.

Timu zingine zilizopo katika kundi hilo ni pamoja na Madagaska na Benin, ambazo zinatafuta nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar 2022.

Katika viwango vya ubora vilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), Tanzania inashika nafasi ya 135, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wenyewe wako katika nafasi ya 65 zikitofautiana kwa nafasi 70.

Tanzania wanashuka Uwanjani bila nahodha wake Mbwana Samata ambaye yuko nchini Ubelgiji akikamilisha usajili wake wakutua katika kikosi cha Royal Antwerp kwa mkopo wa miaka minne kutoka FenerbahceFC ya Uturuki.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen, alisema kuwa kikosi chake kiko kwenye hali nzuri wachezaji wote 23, walioondoka wana nafasi yakupambana na kuipatia timu matokeo ili kuanza vema harakati zakutafuta tiketi ya kutua Qatar.

“Utakuwa mchezo mgumu hasa kwa upande wetu, Congo ni timu nzuri ina wachezaji wazoefu wanaocheza katika Ligi kubwa ulaya lakini kwa maandalizi tuliyofanya naamini tutaenda kufanya vizuri,” alisemaPoulsen.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ea89b429745026ec146e06f682776b4b.jpeg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi