loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simba kuzindua jezi Jumamosi

Simba kuzindua jezi Jumamosi

TIMU ya Simba inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa jezi zake za msimu wa 2021/22, Jumamosi hii katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam,  tukio ambalo litaanza saa 1:00 hadi saa 3:00 usiku.

Simba ambayo iliingia mkataba wa Sh bilioni 2 na Kampuni ya Vunjabei inatarajiwa kuweka wazi jezi zote itakazotumia kuanzia zile za mechi za michuano ya ndani na nje ya nchi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo,  ambavyo vitakuwa na nembo ya Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wawe na subira, kwani jezi za msimu mpya wa Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam, ziko tayari.

Naye Mkurugenzi wa Vunjabei, Fred Ngajiro, alisema kuwa anaitaka kuifanya Simba kuwa klabu ya kibiashara,  kwani tayari wameandaa jezi za aina saba tofauti, na jezi hizo zitapatikana siku hiyo hiyo baada ya uzinduzi na maduka yote ya Vunjabei yatafanya biashara kwa saa 24.

Alisema  kuwa kutakua na mfumo wa manunuzi mtandaoni kwa kutumia mitandao ya kijamii ya Simba AP na ile ya Vunjabei.

“Nafahamu mashabiki wa Simba wana hamu na jezi mpya kama unavyojua Vunjabei inamilikiwa na vijana na sisi tunaenda kuwapa heshima vijana.

“Nimeona jezi nyingi zikisambazwa kuwa ndio zitakazotumiwa na Simba msimu ujao, lakini zote hakuna hata moja, ambayo inafanana na dizaini yetu kutokana na usiri wa kazi yetu mashabiki watarajie jezi nzuri zaidi,” alisema Vunjabei.

Vunjabei alimalizia kwakusema kuwa anatoa ofa kwa mashabiki wa Simba watakao nunua tiketi za Simba Day, basi watapewa punguzo la bei yajezi ilikuwapa fursa ya kwenda uwanjani wakiwa wamevaa jezi hizo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/58fe9305e7399e270868f72574e20503.jpeg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa na Abdallah Mashaka (Tudarco)

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi