loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia aidhamini Cecafa kwa  Dola za Marekani 100,000

Rais Samia aidhamini Cecafa kwa Dola za Marekani 100,000

RAIS Samia Suluhu ametoa Dola za Marekani 100,000 kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati  (CECAFA).

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema fedha hizo zitatumika kwa zawadi za washindi pamoja na kununua tuzo.

“Mgawanyo wa fedha hizo bingwa atapata Dola 30,000, mshindi wa pili Dola 20,000 na mshindi wa tatu Dola 10, 000,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema pia kutakuwa na zawadi ya mchezaji bora, kocha bora na mwamuzi bora.

Rais Samia alitangaza kudhamini mashindano hayo mwezi uliopita Ikulu, Dar es Salaam kwenye hafla ya kuipongeza timu ya taifa ya soka ya U23 iliyotwaa ubingwa wa CECAFA, nchini Ethiopia.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b6ebf9e53e5e2a8731b0505351f34e5e.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi