loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia amwaga mamilioni Cecafa

Samia amwaga mamilioni Cecafa

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa Dola za Marekani 100,000 kwa ajili ya michuano ya wanawake kwa ngazi ya klabu ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa michuano hiyo kuanzia sasa itaitwa Cecafa Samia Women Cup (Kombe la Samia la Cecafa kwa Wanawake).

Akizungumza akiwa jijini Nairobi nchini Kenya juzi, Mwenyekiti wa Cecafa, Wallace Karia alisema fedha hizo tayari zimeshawekwa benki. Karia pia ni Rais wa TFF.

Taarifa ya TFF jana, ilitoa mchanganuo wa matumizi ya fedha  hizo kwamba zitatumika kwenye zawadi za fedha taslimu kwa timu na washindi mmoja mmoja, na pia zitatumika katika manunuzi ya tuzo mbalimbali zitakazotolewa na gharama nyingine zinazohusiana na tuzo.

Taarifa hiyo ya TFF ilifafanua kuwa bingwa atapata dola za Marekani 30,000, mshindi wa pili dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000. Iliongeza kwamba pia kutakuwa na tuzo za kocha bora, wachezaji bora na mwamuzi bora.

Awali, jana gazeti hili lilimkariri Karia akiwa Nairobi akieleza kuwa Rais Samia ametoa Sh milioni 60 kwa ajili ya mashindano hayo ambazo zitatumiwa kwa zawadi ya mshindi wa kwanza Sh milioni 30,000, wa pili Sh milioni 20,000 na wa tatu Sh milioni 10,000. Pia alisema kutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora, kipa bora na mfungaji bora.

Hata hivyo, imebainika kuwa fedha alizotoa Rais Samia kwa ujumla wake ni dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 230), na siyo Sh milioni 60 kama gazeti hili lilivyoripoti jana. 

Udhamini aliotoa Rais Samia ni zawadi kubwa kuliko mashindano yote ya Cecafa. 

Timu nane zinashiriki mashindano hayo katika Jiji la Nairobi ambako Tanzania Bara inawakilishwa na Simba Queens na Zanzibar inawakilishwa na New Generation.

Katika hatua nyingine, michuano hiyo inaendelea leo ambako Simba Queens itakuwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani kucheza na FAD ya Djibouti.

Bingwa wa michuano hiyo atawakilisha Cecafa kwenye michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyopangwa kufanyika Misri baadaye mwaka huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7ae7b235a02c23ef57a787191b71e2c4.jpeg

MABAO mawili ya kiungo mshambuliaji Benard ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi