loader
Stars yapata sare ugenini

Stars yapata sare ugenini

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana imeanza kwa sare ya 1-1dhidi ya timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC), katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar  uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi.

Katika mchezo huo wa Kundi J, DRC walimiliki mpira kwa vipindi vyote na dakika ya 23 walipata bao lililofungwa na Mbokani baada ya kuwahadaa mabeki wa Taifa Stars.

Licha ya wenyeji kutawala mchezo, wachezaji wa Taifa Stars walifanya mashambulizi na dakika ya 35, Simon Msuva alisawazisha bao kwa shuti akiwa nje ya eneo la penalti, akiunganisha pasi ya Reliant Lusajo na kufanya kwenda mapumziko 1-1.

Kipindi cha pili kocha Kim Poulsen alimtoa Dickson Job na Novatus Dismas na kuwaingiza Mudathir Yahya na Bakari Mwamnyeto kwa lengo la kuimarisha kiungo na sehemu ya ulinzi.

Lengo la kocha lilifanikiwa kwani licha ya DRC kumiliki mpira wakiwa kwenye uwanja wao walishindwa kupenya eneo la Stars kutokana na uimara wa kiungo na kushambulia kwa kushtukiza.

Mchezo ujao Taifa Stars itacheza na Madagascar, Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Taifa Stars ipo Kundi J pamoja na DRC, Madagascar na Benin. Mchezo mwingine wa kundi hilo ulitarajiwa kuchezwa jana usiku ukiwakutanisha Madagascar na Benin. 

Mechi nyingine za jana, Kenya ikiwa nyumbani ililazimishwa suluhu na Uganda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/aa1256211f0493aba1d250c67242494a.jpeg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi