loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nabi: Mchezo na Rivers mgumu

Nabi: Mchezo na Rivers mgumu

KOCHA Mkuu wa Yanga Nassredine Nabi, amesema mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Rivers ya Nigeria utakuwa mgumu kutokana na aina ya maandalizi aliyo nayo.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Rivers Septemba 12 mwaka huu, katika mechi ya hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nabi alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na aina ya maandalizi ya kikosi chake kwani kalenda ya Shirikisho la soka la kimataifa, FIFA,  imeharibu mipango yake kwa vile baadhi ya nyota wake wameenda kuwakilisha nchi zao. 

Yanga inaendelea kujifua ikiwa kambini Kigamboni kujiandaa na msimu mpya wa Ligi  Kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nabi alisema, kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata timu yake kutoka kwa Zanaco katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa mwishoni mwa wiki iliyopita, kimeizindua na hivyo sasa amewekeza nguvu kubwa katika maandalizi.

Yanga mara ya mwisho kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka, 2019 ilipoondolewa na Zesco ya Zambia kwa mabao 2-1,  baada ya kutoka sare ya 1-1 nyumbani kisha  kupoteza 1-0 ugenini.

Nabi alisema, mchezo dhidi ya Zanaco umemuonesha aina ya wachezaji alio nao kikosini hivyo anaenda kuyafanyia kazi mapungufu hayo kabla hajashuka uwanjani kuwakabili Rivers. 

"Tumecheza michezo miwili ya kirafiki mmoja wa kimtaifa dhidi ya Zanaco FC, umenisaidia kuona mapungufu ya kikosi changu nitatumia siku zilizobaki kabla ya kucheza na Rivers.

“Naendelea kutengeneza  muunganiko mzuri baina ya wachezaji wangu ambao wengi ni wapya, lakini pia nahitaji kupata mechi nyingine ya kirafiki ya kujiweka fiti zaidi na kupata mwanga wa kuona mapungufu na ubora wetu," alisema Nabi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8da3705161a8c836574374bc512ca5fe.jpeg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi