loader
Simba yatangaza uzi mpya

Simba yatangaza uzi mpya

Klabu ya Simba imetangaza jezi mpya za msimu wa 2021/2022, zitakazoanza kuuzwa leo ikiwa ni siku moja kabla ya tarehe ya uzinduzi wa jezi hizo uliopangwa kufanyika Septemba 4, 2021.

Akizunguma na waandishi wa habari leo, Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga alisema tabia ya kuvujisha jezi kwa klabu hiyo utakuja kusababisha mfarakano.

“Kuna timu kama Coast Union, wametoa jezi lakini hazikuvuja, imefika Simba jezi zimevuja, kwanini uvujishe jezi ya timu? Tukianza utani wa kuvujisha jezi tunakoenda itakuwa ni vita,”alisema Kamwaga.

Kamwaga alitumia nafasi hiyo kutangaza viingilio vya mchezo wa Tamasha la Simba Day litakalofanyika September 19 Uwanja wa Mkapa.

Alitaja viingilio hivyo kuwa 200,000 kwa viti vya Platinum, 30,000, VIP B & C, 20,000 na Mzunguko ni 5,000.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/78474821fbd9b6df15ce27a949eb8e7d.jpg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi