loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kongole Stars msibweteke safari bado mbichi kabisa

Kongole Stars msibweteke safari bado mbichi kabisa

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars imeanza vema harakati za kutafuta nafasi ya kufuzu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar, kwa kupata pointi moja ugenini baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mchezo huo wa Kundi J ulichezwa katika Uwanja wa TP Mazembe, jijini Lubumbashi, nchini Congo, matokeo hayo yamewashangaza wengi kutokana na pengo lililopo baina ya timu hizo mbili.

Licha ya kumkosa nahodha Mbwana Samata na msaidizi wake, John Bocco, timu ilikuwa kwenye mabega ya Simon Msuva, ambaye alihakikisha hatuondoki mikono mitupu nchini Congo.

Kwa matokeo hayo, Taifa Stars imeonyesha wazi kuwa mwaka huu imedhamiria kufanya vizuri na kuwatoa kimaso maso watanzania .

Baada ya sare hiyo, Taifa Stars inarudi nyumbani kuwakabili Madagascar, katika mchezo wa pili wa kutafuta nafasi ya kukaa juu kwenye msimamo wa Kundi J, ambalo pia lina timu za Congo na Benin.

Hivyo basi, wachezaji wa Taifa Stars na benchi lao la ufundi chini ya Kocha Kim Poulsen halina budi kufahamu kuwa ndio kwanza safari bado mbichi kabisa hivyo sare waliyoipata dhidi ya Congo isiwavimbishe kichwa.

Mchezo dhidi ya Madagascar utakuwa mgumu kutokana na timu hiyo kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Benin, hivyo watakuja wakipania kupata matokeo mazuri.

Tunafarijika na hatua ya Poulsen kuwa ataingiza kikosi chake uwanjani akilenga kushambulia ili kuwa na uhakika wa kupata matokeo ili kujikusanyia pointi na kusogea juu ya msimamo.

Poulsen amesema wameondoka nchini Congo, wakiwa na lengo la kupata ushindi, katika mchezo ujao hali inayotia moyo na kujenga imani kuwa timu yetu ya taifa imepania kufanya

vizuri katika kundi lake tukiwa tunatafuta nafasi ya kufuzu michuano mikubwa duniani na kufuzu kwa fainali zake nchini Qatar.

Kwa mchezo uliooneshwa na kikosi cha Stars katika mechi ya kwanza, hatuna shaka kwamba inao uwezo wa kupata matokeo mengine mazuri nyumbani ambako itakuwa ikipata sapoti kutoka kwa mashabiki wetu.

Ili haya yote yaweza kupatikana, ni lazima Taifa Stars ijipange kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho hakuna kuridhika hadi pale tutakapo timiza malengo yetu ambayo ni kufuzu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Natamka wazi kuwa kufuzu kwa fainali za Qatar 2022 inawezekana, lakini kama kutakuwa na nidhamu ya hali ya juu mchezoni kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Kikosi cha Stars tangu kiwe chini ya mikono ya Poulsen, hatuna shaka kuwa uwezekano wa kupata matokeo dhidi ya Madagascar upo japokuwa mchezo wa soka una matokeo ya aina tatu kushinda, kufungwa na kutoka sare.

Lakini pia hili litawezekana iwapo kama Watanzania wote wataendelea kuiunga mkono timu yao na kupewa sapoti inayohitajika basi wachezaji wataongeza juhudi zaidi.

Wakati tukiipongeza Taifa Stars kwa kuanza vema harakati za kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za kombe la dunia naitakia kila la heri katika mchezo wa pili dhidi ya Madagascar.

Lakini namkumbusha kocha Kim na jeshi lake wafahamu kuwa safari ndio kwanza imeanza na kuna safari ndefu mbele hivyo hawapaswi kubweteke wanapaswa kukaza buti ili waweze kuweka rekodi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2022.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/08635a881375c0d485b809362e171c2c.png

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi