loader
Dstv Habarileo  Mobile
Stars yaipania Madagascar

Stars yaipania Madagascar

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amesema kuwa baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), timu yake imepania kuibuka na ushindi katika mchezo ujao dhidi ya Madagascar utakaofanyika nyumbani.

Taifa Stars itakutana na Madagascar Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo mwingine wa kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Alisema kuwa watajipanga vizuri kuhakikisha wachezaji wake watapambana ili kupata ushindi, na kwa ushirikiano wa mashabiki hakuna shaka kuwa, watafanya vizuri.

Alisema kuwa ushindi dhidi ya Madagascar ni muhimu, kwani utaiwezesha timu hiyo kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua inayofuata ya kufuzu kwa fainali hizo za Kombe la Dunia, ambazo Tanzania haijawahi kushiriki hata mara moja.

Aidha, Kim aliwapongeza wachezaji wake kwa sare hiyo katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi juzi.

Taifa Stars ilitanguliwa kufungwa na DRC na baadae mshambuliaji Simon Msuva alisawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.

Akizungumza kwa njia ya mtandao jana, Poulsen alisema wachezaji wake walipambana wakati wote na walionesha kiwango kizuri, na matokeo yake wameondoka ugenini na pointi moja.

“Mchezo ulikuwa mgumu kwa sababu pia wapinzani wetu walikuwa bora na walimiliki mpira kipindi cha kwanza na kupata bao ambalo tulisawazisha,”

“Kwa namna wachezaji walivyopambana wanastahili pongezi kwa kuwa wamefanya kazi kubwa dhidi ya mpinzani wetu ambao walikuwa imara karibu muda wote wa mchezo japo makosa yalikuwepo, lakini mengine tuliyafanyia kazi kipindi cha pili,” alisema Poulsen.

Taifa Stars wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na nguvu kutokana na kuwa na pointi moja, lakini wapinzani wao Madagascar juzi walifungwa 1-0 nyumbani na Benin.

Kwa maana hiyo, Benin inaoongoza ikiwa na pointi tatu, DRC na Tanzania zina pointi moja kila mmoja na Madagascar haina kitu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/28722d9dc96f84b2d2ded48538d1fc24.jpeg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi