loader
Hitimana afurahia  usajili Mtibwa    

Hitimana afurahia usajili Mtibwa    

KOCHA mpya wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amesema amefurahishwa na usajili uliofanywa na timu hiyo na ana amini utakwenda kurudisha makali ya timu hiyo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1999/2000.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Thiery kurejea katika kikosi cha Mtibwa Sugar, awali alijiunga na timu hiyo akitokea Namungo FC akichukua nafasi ya Zuberi Katwila na sasa anachukua mikoba ya Mohamed Badru aliyemaliza mkataba wake.

Mtibwa Sugar inaendelea na mazoezi chini ya Shaban Nditi, ikisubiri kurejea kwa Thiery ambaye yuko nchini Burundi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Thiery alisema malengo yake ni kuisaidia Mtibwa Sugar kufanya vizuri katika mashindano yote itakayoshiriki msimu ujao utakaoanza Septemba 29, mwaka huu.

“Nimefurahi kurejea tena Mtibwa Sugar ni timu nzuri yenye rekodi nzuri ninakwenda kufanya kazi ambayo itairudisha  timu katika kiwango kilichozoeleka.”

“Sitaki kukumbuka nini kilitokea wakati uliopita, msimu huu tunakuja kivingine mashabiki wa Mtibwa Sugar watarajie mambo mazuri kutoka katika kikosi chao,” alisema Thiery.

Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Mtibwa Sugar msimu huu ni, Said Ndemla na Ibrahim Ame kutoka Simba, Hassan Kibailo, Abdi Banda na Steven Nzigamasabo kutoka Burundi.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fa948095daa2cb5c925a3f9953bb9071.jpg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Na Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi