loader
Dstv Habarileo  Mobile
Diamond, Mobetto,  Fahyma wang’ara Nigeria

Diamond, Mobetto, Fahyma wang’ara Nigeria

WASANII wa Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobetto na Fahyma wameibuka washindi katika tuzo za Scream All Youth Awards 2021 zilizotolewa nchini Nigeria juzi.

Tuzo hizo hutolewa kwa vijana wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali Afrika na ni za nane kufanyika.

Diamond Platnumz alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka, Hamisa Mobeto katika kipengele cha chapa bora yenye ushawishi ya mwaka na  Fahyma katika kipengele cha mshawishi bora katika mitandao ya kijamii.

Diamond alichuana na wasanii kama Mbosso, Mario, Darassa wote wa Tanzania, Pallaso na Fik Fameica wa Uganda, Rema na Omah Lay wa Nigeria.

Fahyma aliwashinda Diva Thee Bawse wa Tanzania, Sharon Ephraim, Opeyemi Kareem, Dk Olufunmilayo, Arinzaany na Twinz The Love wote wa Nigeria.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/93d60418ee1da9b7bef51d0c9d3dba3b.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Na Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi