loader
Billnass: Nandy  ameacha alama

Billnass: Nandy ameacha alama

MSANII wa Bongo fleva, William Lyimo ‘Billnass’  amesema msanii Faustina Charles ‘Nandy’ kufanya tamasha kubwa lililowakutanisha wasanii wakubwa wa ndani na nje ya nchi ni jambo kubwa ambalo litaacha alama kwa mashabiki kutokana na uthubutu wake.

Billnass ambaye hakuwahi kuonekana katika shoo tatu za Nandy Festival zilizofanyika Kigoma, Mwanza na Zanzibar, alijitokeza juzi katika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam juzi, Billnass alisema tamasha hilo ni jambo kubwa kufanyika hapa nchini hasa kwa binti kama yeye kufanya kitu kubwa ambacho kimeungwa mkono na wasanii wakubwa, lakini pia waandishi wa habari wamefanya kazi kubwa kuhakikisha linafanyika kwa ukubwa.

“Naamini bila wasanii na mashabiki na waandishi wa habari kusapoti tamasha hili lisingekuwa kubwa kama hivi, lakini pia muamko wake mawazo  na utayari vimesaidia kufanya jambo hili kubwa la kihistoria.”

“Sio kila mtu anaweza kuandaa shoo, hivyo kuona mtu ameandaa kitu kikubwa kama hiki anaacha alama, kuna vitu vingi vya kujifunza kwa wasanii wengine wamtazame Nandy kama mfano,” alisema Billnass.

Wasanii walioshiriki tamasha hilo ni Juma Kassim ‘Nature’,  kundi la Weusi linaloundwa na John Simon ‘Joh Makini’, Nickson Simon ‘Niki wa Pili’, Lord Eyes na G nako, Astelina Sanga ‘Linah’, Clayton Chipando ‘Baba Levo’ na kutoka Kenya ni Wilson Abubakar ‘Willy Paul’.

Wengine ni kundi la Mabantu linaloundwa na Muuh Kajo na Twaah Kane, Baddest, Herri Sameer ‘Mr Blue’, Juma Mkambala ‘Jux’ na Frank Felix ‘Foby’, Whozu, Nally Chuga Princess,  Sholo Mwamba, Rosa Ree, Dulla Makabila na  Saraphina.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ef1f0799c50c25870052051e7019fa0b.png

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Na Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi