loader
Dstv Habarileo  Mobile
Donda ya Kanye  yakimbiza England

Donda ya Kanye yakimbiza England

ALBAMU ya muziki wa Hip hop ya Kanye West  inayoitwa 'Donda' imeshika namba moja katika chati za mauzo England na kuwa albamu ya tatu ya mkali huyo kushika namba moja baada ya  baada ya Graduation alioachia 2007 na Yeezus ambayo aliachia mwaka 2013.

Ikiwa ndio wiki ya kwanza tangu ilipoingia sokoni, tayari Donda imesikilizwa mara milioni 33.4 duniani kote.

Donda imeweka rekodi nyingine kwenye burudani baada ya kuzinduliwa mara mbili katika majiji ya Atlanta na Chicago, Marekani, lakini kubwa zaidi ni kitendo cha kufuta baadhi ya mistari iliyoimbwa na rapa Jay Z.

Hii ni albamu ya 10 kwa Kanye West na imepewa jina la ‘Donda’ kama heshima kwa mama yake Donda West, Profesa aliyekuwa akifundisha Chuo Kikuu cha Chicago ambaye alifariki mwaka 2007 akiwa na miaka 58 kwa shambulio la moyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/503da3f883027b8584ad40bea00b4be7.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi