loader
Simba Queens yatolewa Cecafa

Simba Queens yatolewa Cecafa

TIMU ya Simba Queens imeondolewa katika mashindano ya Samia Super Cup ya Cecafa kwa ajili ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa wanawake, baada ya kufungwa 2-1 na Vihiga ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo nchini humo jana.

Mchezo huo uliokuwa na presha kubwa, ambapo wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 65 lililofungwa na Maureen Achieng kwa kichwa na mpira kumshinda kipa wa Simba, Zubeda Mgunda.

Simba walirejea mchezoni na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 70 kupitia kwa Aisha Juma ambaye alifunga kwa shuti kali akimalizia mpira uliomshinda kipa wa Vihiga.

Zikiwa zimebakia dakika mbili mpira kumalizika, Vihiga walifunga bao la ushindi lililowekwa kimiani na mshambuliaji Jentrix Shikangwa kwa kichwa akimalizia vema mpira wa adhabu uliopigwa kutoka upande wa kulia wa uwanja.

Simba Queens walitinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yake miwili ya Kundi A dhidi ya PVP ya Burundi kwa mabao 4-1, kisha kuibugiza  FAD  FC  ya  Djibout 10-0.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/db34e3074fa7d942aa635384dd90fede.jpg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: Na Amina Jumanne, TUDAR

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi